‎
Na Mwandishi Wetu, Handeni ‎ ‎ 

Mifugo 148,172 katika Halmashauri ya Mji Handeni, mkoani Tanga, inatarajiwa kuchanjwa dhidi ya magonjwa ya kideri, sotoka na mapafu, kupitia kampeni ya kitaifa ya chanjo ya mifugo. ‎ ‎

Akizindua kampeni hiyo Agosti 22, 2025 katika Kata ya Malezi, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Salum Nyamwese, amewahimiza wafugaji wote wa Halmashauri hiyo wajitokeze kishiriki zoezi hilo la kitaifa ili kukabiliana na magonjwa ya mifugo. ‎ ‎

Kwa upande wake, Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri hiyo, Aldegunda Matunda, amesema kati ya idadi hiyo ya mifugo; ng’ombe ni 38,006, mbuzi 25,356, kondoo 9,567 na kuku 75,243. ‎ ‎

Amesema Halmashauri hiyo inakadiriwa kuwa na wafugaji wapatao 34,484 na kwamba sekta ya mifugo imekuwa ikichangia asilimia 21.78 ya mapato ya Halmashauri kwa mwaka, sambamba na kuinua kipato cha wananchi. ‎ ‎

“Halmashauri imepokea mgao wa chanjo za ruzuku kutoka serikali kuu pamoja na vitendea kazi kwa ajili ya kudhibiti magonjwa ya mifugo. Tumejipanga kutoa elimu kwa wataalamu wetu walioko mashinani ili kusimamia zoezi hili ipasavyo,” amesema Matunda. ‎ ‎

Amebainisha kuwa chanjo zitakazotolewa ni ya homa ya mapafu kwa ng’ombe (CBPP), homa ya sotoka kwa mbuzi na kondoo (PPR), na kideri kwa kuku, katika kata zote 12 za Halmashauri hiyo. ‎ ‎

“Katika zoezi hili, mfugaji atachangia nusu ya gharama ya chanjo, huku utambuzi wa mifugo ukitolewa bure kabisa,” amesema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...