Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania (SLR) umetumia kiasi cha Shilingi Milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki Kijiji cha Ikulwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Mkoani Katavi.

Akizungumza wakati wa mahojiano maalum Agosti 6, 2025, katika Viwanja vya Maonesho ya 32 ya kitaifa ya Wakulima, Wafugaji (Nanenane) Jijini Dodoma, Katibu wa Kikundi cha Upendo Daima Ikulwe kinachojihusisha na uhifadhi wa mazingira Wilayani Mpimbwe, John Magoma amesema ujenzi huo umeongeza thamani mazao ya nyuki na kuongeza uhakika wa masoko.

Magoma amesema tangu kuanza kwa utekelezaji wa shughuli za mradi wa SLR Kijiji hapo mwaka 2023, wananchi wengi wamehamasisha katika masuala ya usimamizi wa uhifadhi wa mazingira kupitia shughuli za uzalishaji mali ikiwemo uvunaji wa mazao ya nyuki.

“Kijiji chetu kabla ya shughuli za mradi kilikuwa na changamoto kubwa ya uharibifu wa mazingira ikiwemo uchomaji moto misitu, uharibifu wa vyanzo vya maji na migogoro ya ardhi...Lakini tangu kuanza kwa mradi, migogoro ya ardhi imekwisha na wananchi wamepata mwamko mkubwa katika uhifadhi wa mazingira” amesema Magoma.

Ameeleza kuwa kupitia uvunaji wa mazao ya nyuki ikiwemo asali, kikundi hicho hadi sasa kimeweza kuuza asali yenye ujazo wa kilo 203 na kuweza kujipatia kiasi cha Shilingi Milioni 2 ambazo zimeweza kunufaisha wanachama 18 wa kikundi hicho.

Amefafanua kuwa kufuatia mafanikio ya mradi, wanajamii katika Kijiji cha Ikulwe wakiwemo wafugaji na wakulima wamekuwa na mwamko na ushirikiano wa pamoja katika kuhimiza mbinu mbadala na endelevu katika urejeshaji na uhifadhi uoto wa asili.

“Uharibifu wa mazingira unachangiwa na shughuli za kiuchumi zisizo endelevu ikiwemo ufugaji holela, ukataji miti ovyo, uvamizi wa maeneo tengefu na vyanzo vya maji, kufuatia elimu tuliyopatiwa kupitia mradi wa SLR wanakijiji kwa sasa tumekuwa mabalozi wa kulinda na kutunza mazingira” amesema Magoma.

Ameeleza Ofisi ya Mradi wa SLR umefanikiwa kukipatia kikundi hicho vitendea kazi mbalimbali ikiwemo mizinga ya nyuki 50 yenye thamani ya Shilingi Milioni 4.2 sambamba na vifaa vingine ambayo ni ndoo, mavazi, viatu, chujio la asali na madumu ya kubebea asali.

Ameongeza kuwa kabla ya kupatiwa vitendea kazi vya kisasa kutoka Mradi wa SLR, kikundi hicho kilikuwa kinatumia dhana duni ikiwemo mizinga ya magogo ambayo ilisababisha uvunaji usio na tija wa mazao ya nyuki na hivyo kutishia uhai wa kikundi hicho cha kijamii cha uhifadhi wa mazingira.

Mradi wa SLR unatekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) kupitia usaidizi wa kitaalamu wa Shirika la Kimataifa la Hifadhi ya Mazingira Asilia (IUCN).

Jumla ya Mikoa mitano (05), Halmashauri saba (07), Kata 18 na Vijiji 54 vinanufaika na Mradi wa SLR ambao unafadhiliwa na Mfuko wa Dunia wa Mazingira (GEF) kwa kipindi miaka mitano (05) kuanzia mwaka 2021- 2025.


Katibu wa Kikundi cha......Bw. akitoa maelezo kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Zuzu iliyopo Jijini Dodoma wakati walipotembelea Banda la Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Mazingira (SLR) kujifunza masuala mbalimbali kuhusu fursa zilizopo katika hifadhi ya mazingira nchini.

(Na Mpigapicha Wetu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...