Na Mwandishi wa NCAA Dodoma.

Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro imetoa wito kwa watanzania kutembelea vivutio vinavyosimamiwa na mamlaka hiyo ili kujifunza masuala mbalimbali kuhusu wanyama na malikale.

Afisa Uhifadhi Mkuu Masoko NCAA, Michael Makombe ameeleza hayo kwa kuwa wananchi wanaotembelea maonesho ya nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nzughuni mjini Dodoma na kuongeza kuwa;

“Tunatumia maonesho haya kuwaelimisha watembeleaji kuhusu upekee wa Ngorongoro kama sehemu yenye utajiri wa vivutio vya utalii, kuwaelezea gharama za kuingia hifadhini, fursa za uwekezaji, uhifadhi shirikishi na historia ya binadamu na makabila yanayoishi kiasili Tanzania ,”alisema Bw.Makombe.

Afisa Uhifadhi Mkuu, urithi wa Utamaduni na Jiolojia PCO Ramadhan Hatibu ameeleza kuwa wananchi wanaotembelea maonesho hayo pia wanapata elimu ya kujua vivutio vya urithi wa utamaduni, chimbuko la binadamu wenye umri wa zaidi ya miaka 3.6 iliyopita, kupata habari za eneo la Olduvai lenye masalia ya viumbe hai walioshi zaidi ya miaka Mil 2 iliyopita na kujua Jamii za makabila ya wamaasai, Wadatoga, Wahadzabe na wairaq ambapo wageni wanaotembelea Ngorongoro wanaweza kuona Jamii za makabila hayo zinavyoishi maisha yao ya asili na kulinda utamaduni wao.

PCO Hatibu ameeleza kuwa Ngorongoro ni eneo muhimu ambalo ni urithi wa dunia ikiwa sehemu pekee katika nchi za Ukanda wa Afrika kuwa hadhi 3 kwa pamoja ambazo World Herritage Site, Biosphere Reserve na Urithi wa kijiolojia (UNESCO Global Geopark) na kutumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi kutembelea hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kujifunza na kuona utajiri wa Dunia uliopo katika hifadhi hiyo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...