MJASILIAMALI Sabri Hamis mwenye makazi yake Zanzibar amejishindia vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Milioni tano baada ya kuibuka mshindi katika jukwaa jipya la kibunifu lijulikanalo ‘Piku’.
Jukwaa hilo la Piku ambalo limzezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam lipo katika mfumo wa mnada unaotoa fursa kwa watanzania kucheza kwa kuweka dau la chini la kipekee na hatimaye kujishindia vifaa mbalimbali vya thamani.
Hamis kupitia jukwaa hilo ameweza kujishindia Television inchi 55, Kiyoyozi na kifaa cha muziki vyote kutoka LG, king’amuzi cha DStv kilicholipiwa mwaka mzima pamoja na kifaa cha internet (router) kilicholipiwa mwaka mzima kutoka Airtel.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja wa Habari na Mawasiliano, Barnabas Mbunda amesema Piku ni jukwaa la kidigitali linalohusisha vijana na watu wazima kunzia miaka 18 na kuendelea ambapo mshiriki anaweza kupakua App ya jukwaa hilo kwenye simu za adroid kwa kuingia kwenye ‘play store’.
Amesema washiriki wanaweza kununua tiketi kwa bei nafuu kuanzia Sh.1,000 kwa tiketi 10, sh 5,000 kwa tiketi 50, sh. 10,000 kwa tiketi 100, na kuendelea hadi sh 100,000, ambapo nafasi ya ushindi huwa kubwa zaidi.
“Tofauti na majukwaa mengine au minada ya kawaida inayojulikana, Piku unafanya kazi kwa njia ya kipekee kabisa kwani mshindi ni yule aliyeweka dau la dogo na la kipekee ambalo halijarudiwa na mshiriki mwingine yeyote. Hii inamaanisha kwamba kila mshiriki ana nafasi ya kipekee ya kushinda bidhaa za thamani kwa gharama ndogo kabisa,” amesema Mbunda
Amesema zawadi kwa washindi hutolewa kila wiki, mwezi, na baada ya miezi mitatu na kwamba jukwaa hilo limezingatia wau wa madaraja yote hasa wa kipato cha chini.
Aidha Mbunda amewahimiza watanzania kupakua app ya Piku na kushiriki ili wawe miongoni mwa washindi wa siku zijazo.
Naye Hamis ambaye ndio mshindi wa kwanza katika jukwaa hilo tangu kuzinduliwa kwake amesema amefurahishwa na ujio la jukwaa hilo lenye lengo la kuwanua vijana na wajasirimali mbalimbali.
“Mimi nimecheza mara moja na nimetumia sh.1000 tu ambayo imeniwezesha kushinda vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Milioni tano, hakika hii ni nguvu ya buku na kweli nimeamini elfu moja ina nafasi ya kubadili maisha yako. Niwaombe watu wapakue hiyo app na kucheza kwani maisha yanaweza kugeuka kwa dau moja tu,” amesema Hamis
Kwa upande wake Mkaguzi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Lucy Katamba amesema jukwaa hilo limechezeshwa vizuri na mshindi amepatikana kwa haki huku akisisitiza kuwa sekta ya michezo inakua na kuchangia maendeleo ya kiuchumi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...