Mkazi wa Masaki na mfanyabiashara Riziki Shaweji(40) na wenzake sita wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakidaiwa kuingiza sampuli za dawa kulevya aina ya Mitragyna Speciosa zenye uzito wa kilo 11.596.
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na wakili wa Serikali, Eric Davies, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga.
Mbali na Shaweji, wengine ni Andrew Nyembe (34), Mariam Ngatila(40) na Ramadhani Said (57) mfanyabiashara na mkazk wa Kifuru.
Wengine ni mkazi wa Oysterbay na mfanyabiashara ni Godwin Maffikiri(40) na raia wa Sri Lanka Jagath Wellalage(46) na Santhush Hewage (25).
Wakili Davies alidai kuwa, washtakiwa walikamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Julai Mosi, 2025 katika bandari kavu ya Said Salim Bakhresa(SSB - ICD) iliyopo eneo la Sokota wilaya ya Temeke, washtakiwa kwa pamoja waliingiza sampuli zenye uhusiano na dawa za kulevya aina ya Mitragyna Speciosa zenye uzito wa kilo 11596, sawa na tani 11.5.
Upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba upande wa mashtaka umeomba mahakama iwapagie tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...