Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) imetajwa kuwa na mchango kwenye suala la Usalama wa chakula nchini kwa kufanya Utafiti unaotoa matokeo yenye kuongeza tija kwa Wakulima katika zama zinazoshuhudiwa uwepo mabadiliko ya tabia nchi.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo anayesimamia Umwagiliaji na zana za Kilimo Mhandisi Athumani Kilundumya na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Edwin Mhende walipotembelea banda la TARI katika Maonesho ya kimataifa ya Kilimo Maarufu kama Nanenane yanayofanyika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Kueleza hilo Dkt. Mhende ametambua kazi kubwa ya ugunduzi wa Mbegu za Mazao mbalimbali inayofanywa na TARI huku akiwasihi Watafiti kuhakikisha Mbegu hizo zinamwezesha Mkulima kuzitumia kwa muda mrefu.
Naye Mhandisi Athumani ameipongeza TARI huku akitaka iongeze kasi katika kusambaza matokea hayo ya Utafiti kwa Wakulima katika maeneo mbalimbali hususani vijijini.
Awali akiwapitisha katika Banda la TARI, Mkurugenzi Mkuu wa TARI Dkt. Thomas Bwana amesema TARI imefanya Utafiti kuanzia afya ya Udongo hadi uongezaji thamani lengo ikiwa ni kuongeza tija katika sekta ya Kilimo suala ambalo amesema katika msimu huu wa Nanenane wanatoa elimu hiyo katika mabanda yote ya TARI kwenye maonesho ya Nanenane yanayoendelea sehemu mbalimbali.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...