* Wampokea kwa shangwe kubwa
 *Ni ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za Madereva Bodaboda na Bajaji

Na Mwandishi Wetu
WAENDESHA Bodaboda na Bajaji wamempokea kwa shangwe Afisa Tarafa Lisekese Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Emmanuel Shilatu, katika ziara yake ya kuzunguka Kata kwa Kata kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili.

Katika mikutano hiyo, Shilatu alisisitiza umuhimu wa kufuata sheria za usalama barabarani na kudumisha uhusiano mzuri kati ya madereva, Jeshi la Polisi na Serikali. Pia aliwahimiza washiriki kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa amani katika Uchaguzi Mkuu ujao, akisisitiza utulivu na mshikamano kama silaha ya kulinda amani ya nchi.

Kwa niaba ya waendesha Bajaji na Bodaboda, Dan Bonge alieleza furaha yao kwa ziara hiyo, akisema ni mara ya kwanza kiongozi mkubwa kuwafikia moja kwa moja ili kusikiliza matatizo yao. Aliongeza kuwa wako tayari kuendelea kushirikiana na Serikali huku akiomba waendelee kupatiwa mikopo ya Halmashauri ili kujiendeleza kiuchumi.

Akijibu hoja hiyo, Afisa Maendeleo wa Kata ya Lukuledi, Musa Soud, aliahidi kushirikiana nao kuhakikisha wanapata mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri. Shilatu naye alisisitiza kuwa mikopo hiyo italetwa kwa uwazi na kuwakumbusha umuhimu wa kurejesha kwa wakati.

Aidha, alimpongeza dereva pekee wa kike aliyeshiriki, akiwahimiza wanawake wengine kuiga mfano huo ili kuondoa dhana potofu kwamba kazi za udereva ni za wanaume pekee.

Ziara hiyo ilihudhuriwa pia na Kamati ya Usalama ya Tarafa, wataalamu wa kata, pamoja na viongozi wa vijiji, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...