Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia leo August 06,2025 akiwa anaendelea kupatiwa matibabu Hospitalini baada ya kuugua ghafla.

Kwa mujibu wa taarifa ya Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson aliyoitoa imesema: “Kwa masikitiko makubwa, naomba kutoa taarifa ya kifo cha kiongozi wetu, mwanasiasa mkongwe na Spika mstaafu wa Bunge, Job Ndugai kilichotokea leo jijini Dodoma.

“Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Jimbo la Kongwa, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.”

Dk Tulia amesema Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na kamati ya mazishi pamoja na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Ndugai amekuwa Spika wa Bunge tangu November 17, 2015 hadi Januari 06, 2022 alipojiuzulu na kuendelea kuwa Mbunge wa Kongwa nafasi ambayo ameendelea kuitetea kwa kuchukua fomu tena mwaka huu ambapo ameshinda kwenye kura za maoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...