Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Morogoro
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Rais Dk.Samia Suluhu leo Agosti 29,2029 ametumia usafiri wa treni ya mwendo kaşi ya SGR akitokea Dar es Salaam kwenda Morogoro kwa ajili ya kuendelea na kampeni za uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Rais Dk.Samia aliondoka na treni ya SGR mapema asubuhi ya leo ambapo katika ratiba yake ya mikutano alikuwa na mkutano wa kampeni katika tarafa ya Ngerengere iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini ,hivyo baada ya kufika kituo cha SGR Ngerengere alishuka na kisha kuelekea katika mkutano wake wa kampeni.
Hata hivyo baada ya kumalizia mkutano wa kampeni aliondoka kwa gari na kisha kupanda tena treni ya SGR kuelekea Morogoro Mjini ambako alikuwa na mkutano mkubwa wa hadhara ambao umehudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Mkoa.
Kwa kukumbusha tu katika kipindi cha miaka minne na nusu ya uongozi Dk.Samia katika moja ya miradi ambayo ameisimamia kuhakikisha inakamilika ni treni ya SGR ambayo ilishakamilika na kuanza safari zake kati ya Dar es Salaam na Dodoma na Ujenzi wa reli hiyo unaendelea kuelekea Tabora hadi Mwanza na mkakati wa Serikali ni kuhakikisha treni ya SGR pia inafika Mkoa wa Kigoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...