Farida Mangube, Morogoro
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema matumizi ya vipimo sahihi ni msingi muhimu wa maendeleo kwa mkulima, mfanyabiashara na Mtanzania kwa ujumla, akisisitiza kuwa Serikali haitaendelea kuvumilia vitendo vya udanganyifu kupitia mizani zisizo sahihi.
Akizungumza katika Maonesho ya Kilimo (Nanenane) Kanda ya Mashariki yanayofanyika katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl. J.K. Nyerere mjini Morogoro, Chalamila alitoa pongezi kwa Wakala wa Vipimo (WMA) kwa kazi nzuri wanayoifanya kuhakikisha haki na usawa vinazingatiwa katika shughuli za biashara nchini.
“Naipongeza sana Wakala wa Vipimo kwa kazi nzuri ya kuhakikisha vipimo sahihi vinatumika katika shughuli mbalimbali, hasa katika sekta ya kilimo na biashara. Wakulima na wafanyabiashara wanapaswa kuhakikisha wanatumia vipimo vilivyohakikiwa kwa mujibu wa sheria ili kulinda haki zao na za wateja wao,” alisema Chalamila.
Aliongeza kuwa matumizi ya vipimo sahihi si tu yanasaidia kuimarisha biashara bali pia yanachochea ustawi wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Aliwataka wakulima na wafanyabiashara kuhakikisha wanawasiliana na Wakala wa Vipimo mara kwa mara ili kupata huduma ya uhakiki wa mizani na vipimo vyao.
“Serikali haitaki kuona wananchi wanadhulumiwa kutokana na mizani za kughushi. Tutawachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kuchezea vipimo kwa manufaa binafsi. Haki ni msingi wa amani, na vipimo sahihi ni sehemu ya haki hiyo,” aliongeza.
Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Vipimo mkoa wa Morogoro, Bw. Phanuel Matiko, alisema maonesho ya Nanenane yamekuwa jukwaa muhimu kwa taasisi hiyo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutumia vipimo sahihi katika shughuli zao za kila siku.
“Tunaendelea kutoa elimu kwa wakulima, wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla juu ya matumizi sahihi ya vipimo. Pia tunafanya ukaguzi na uhakiki wa mizani hapa maoneshoni ili kuhakikisha kila anayeshiriki anafuata sheria,” alisema Matiko.
Matiko aliongeza kuwa Wakala wa Vipimo umejipanga kuwafikia wakulima hadi ngazi ya vijiji kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa, kwa lengo la kuwasaidia kuendesha shughuli zao kwa ufanisi na uaminifu.
“Kwa mfano, wakulima wengi wanapouza mazao yao wanapimwa kwa kutumia vipimo visivyo sahihi. Tunapowaelimisha na kuwapatia huduma za uhakiki, tunawawezesha kujilinda dhidi ya udanganyifu na kuongeza tija katika kazi zao,” alisema.
Maonesho ya Nanenane yameendelea kuwa kivutio kwa taasisi mbalimbali za umma na binafsi kuonesha teknolojia, bidhaa na huduma mbalimbali zinazolenga kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...