CHUO  Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia Idara ya Sayansi ya Udongo na Jiolojia kimesisitiza kuwa ni muhimu kwa mkulima anayelenga kulima kwa tija kuhakikisha anapima afya ya udongo pamoja na afya ya mbegu atakazozitumia kabla ya kuanza shughuli za kilimo, ili kuepuka hasara na kuongeza ufanisi wa uzalishaji.

Dkt. Hellen Kayagha kutoka SUA amesema katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea, Chuo hicho kinatoa huduma ya bure ya upimaji wa afya ya udongo, mimea na mbegu.

Amesema huduma hiyo inatolewa kwa wakulima na wageni mbalimbali wanaotembelea banda la SUA, ambapo sampuli zinapokelewa na majibu hutolewa ndani ya saa moja tu, hapo hapo bandani.

“Kwanini ni muhimu mkulima kupima udongo, kwa sababu inamsaidia kufahamu kiasi cha virutubisho kilichopo katika udongo na inampa uwezo wa kujua aina ya mbolea anayotakiwa kutumia na aina gani ya virutubisho ambavyo vinatakiwa kuongezwa kwenye udongo wake ili aweze kulima kwa tija na kupata mazao bora na yenye afya bora,” amesema Dkt. Kayagha.

Kwa upande wa mbegu, amesema mkulima anapoangalia afya ya mbegu anazotumia atakuwa na uhakika wa mbegu anayopanda inaota kwa kiasi gani shambani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...