Vodacom Tanzania, kupitia kitengo cha Vodacom Business kinachoshughulika na wafanyabiashara wakubwa pamoja na wadau mbalimbali wa michezo, wamekabidhi tuzo na zawadi kwa washindi tofauti wa mashindano ya golf yaliyofanyika katika uwanja wa TPDF Lugalo jijini Dar es Salaam, tarehe 2 Agosti mwaka huu.

 Hafla hiyo ilikuwa sehemu ya mashindano ya Vodacom Corporate Masters, yaliyolenga kuhamasisha ushiriki wa wadau kutoka sekta mbalimbali kupitia michezo ya kijamii kama golf. 

Tuzo hizo zilitolewa kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoto wa kike na wa kiume, wanawake, wanaume pamoja na wachezaji wa golf waliobobea kutoka mashirika tofauti. Kupitia tukio hili, Vodacom iliendeleza dhamira yake ya kuunga mkono michezo, kukuza vipaji na kudumisha uhusiano wa kijamii na wadau wake wa karibu.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Ushirikiano kutoka Vodacom Tanzania Joseph Sayi ( wa pili kushoto) akimkabidhi tuzo moja ya washindi wa tuzo ya gofu ya kupiga mbali Bw. Ali  Mamdouhi ( wa pili kulia). Tukio hili limefanyika jana wakati wa ugawaji wa tuzo ulliofanyika na Vodacom Tanzania jijini Dar es salaam.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...