Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa wito kwa wakulima na wavuvi kutumia taarifa za hali ya hewa ili kuleta tija na kuongeza kipato. Wito huo umetolewa kwenye Maonesho Nanenane 2025 yanayofanyika katika Viwanja vya Dole Kizimbani, Zanzibar.
Mkurugenzi wa TMA Ofisi ya Zanzibar, Ndg. Masoud Makame Faki, akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Banda la TMA aliwahimiza wakulima na wavuvi kufuatilia utabiri wa kila siku, utabiri wa msimu pamoja na tahadhari za hali mbaya ya hewa zinazotolewa na Mamlaka,kwani mkulima hawezi kupata utajiri au ongezeko la pato bila kutumia taarifa za hali ya hewa.
Kaulimbiu ni “Kilimo ni utajiri, Tunza Amani, Lima kwa ubunifu”.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...