Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Chemba
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ametoa ahadi ya Ujenzi wa barabara ndani ya Wilaya ya ndani ya Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma ikiwemo barabara ya Chemba - Soya yenye urefu wa kilometa 32.
Kwa mujibu wa Dk.Samia ni kwamba barabara hiyo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu hivyo amesema ahadi yake ni kwamba barabara hiyo inaenda kutengenezwa kwa kiwango ambacho itakuwa inapitika kwani ni barabara muhimu katika uchumi.
“Barabara hiyo ya Chemba-Soya ni tegemeo kwa shughuli za minada inayofanyika kila Jumapili ambayo inaingiza kiasi kikubwa cha fedha ndani ya halmashauri lakini na wafanyabiashara wadogo na wafugaji wanaitegemea kwa kiuchumi.”
Akizungumza barabara ya Kwamotoro - Mpende - Kasakai - Ilahoda na zingine tatu za ndani ya wilaya hiyo, ameahidi kuangalia uwezekano Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini(TARURA) kuiboresha ili itumike katika kipindi chote.
Pia amesema ipo barabara ya Tanga - Handeni - Kiberashi wamemaliza upembuzi yakinifu na utekelezaji wake utaanza mwaka huu huku akisisitiza barabara hiyo inakwenda kujengwa.
“Lakini kuna ahadi nyingine aliyoitoa mpendwa wetu Dk. Magufuli ya kujenga soko na stendi ndani ya Mji wa Chemba, hii nayo tunakwenda kuifanyia kazi kuhakikisha tunamaliza adha hii ya soko na stendi.Kwa upande wa ujenzi wa bwawa la Farkwa unaendelea vizuri nasi tutaendelea kuhakikisha linamalizika…
“Kwasababu tunalitegemea kwa Mji wa Dodoma ambao sasa ni mji mkubwa wa nchi yetu, uhamiaji umeongezeka, mahitaji ya maji ni makubwa mno. Bwawa kama hili ndilo litakalotuokoa, tutahakikisha linamalizika ili tupate maji ya kutosha ndani ya Mji wa Dodoma.”
Pamoja na Maelezo hayo Rais Samia amesema kuwa wananchi wa Chemba wanajua Kazi iliyopo mbele yao ni kuzima rangi zote na kuwasha rangi kijani ya CCM na kauli mbiu yao katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu inasema “KAZI NA UTU TUNASONGA MBELE”.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...