Wananchi wa Mji Mdogo wa Lalago,Maswa Mashariki wilayani Maswa wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi wakati akiwahutubia kwenye mkutano mdogo wa hadhara leo Jumatano Septemba 3,2025,wakati akimalizia mkutano wake wa mwisho wa Kampeni mkoani Simiyu.

Katika mkutano huo wa kampeni,Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi aliwanadi Wabunge wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Maswa Mashariki,Dkt.George Vernance Lugomela na Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi,Mashimba Mashauri Ndaki pamoja na madiwani .

Pamoja na mambo mengine Balozi Dkt.Emmeanuel Nchimbi amekuwa akiinadi Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM Rais Dk.Samia Suluhu,Mgombea mwenza wa Urais,wabunge na madiwani wa Chama hicho.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...