Kampeni za uchaguzi katika Jimbo la Kwimba zimezinduliwa kwa nguvu na hamasa kubwa leo katika Kata ya Hungumalwa, ambapo wananchi zaidi ya 7,000 walihudhuria mkutano wa hadhara uliojaa shangwe na ari ya ushindi.
Katika uzinduzi huo, Shija Malando alitambulishwa rasmi kuwa Mgombea Udiwani Kata ya Hungumalwa, huku Cosmas Bulala akitangazwa kama Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kwimba.
Mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Ndugu Michael Lushinge (Smart), ambaye alisisitiza mshikamanano, mshikamano na ari ya ushindi wa chama katika uchaguzi ujao.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi na wagombea mbalimbali wakiwemo:
- Madiwani wa kata zote 30 za Wilaya ya Kwimba (ambayo ina majimbo mawili: Kwimba na Sumve).
- Moses Bujaga, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Sumve.
- Wagombea Udiwani viti maalum.
- Wagombea Ubunge viti maalum Mkoa wa Mwanza.
- CDE Seth B. Masalu, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mwanza.
- Mhe. Kasalali Mageni, Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumve.
- Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mwanza.
Wananchi walionyesha imani kubwa kwa wagombea wao na kuahidi kushiriki kikamilifu katika kampeni na uchaguzi, kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa wagombea wote wa CCM katika jimbo hilo.
Kijana Cosmas Bulala, mgombea Ubunge wa Jimbo la Kwimba na comrade Shija Malando Mgombea Udiwani Kata ya Hungumalwa wakiwasili kwa Chopa eneo la tukio na kuzua msisimko wa aina yake
Kwa unyenyekevu mkubwa kijana Cosmas Bulala, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kwimba, akiomba kura kwa wananchi
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Ndugu Michael Lushinge (Smart) akimnadi na kumuombea kura kijana Cosmas Bulala, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kwimba kwa wananchi
Uzinduzi wa kampeni za uchaguzi katika Jimbo la Kwimba zimeacha alama yankudumu baada vya kuzinduliwa kwa nguvu na hamasa kubwa atika Kata ya Hungumalwa, ambapo wananchi zaidi ya 7,000 walihudhuria mkutano wa
Katika uzinduzi huo wa kihistoria, kijana Cosmas Bulala alitambulishwa rasmi kama kama Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kwimba huku comrade Shija Malando akitambulishwa rasmi kuwa Mgombea Udiwani Kata ya Hungumalwa uliojaa shangwe na ari ya ushindi.
Wagombea hao, ambao walitua kwa Chopa na kuzua taharuki ya shangwe wametajwa kuwa tegemeo kubwa sana katika jimbo hilo.
Mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Ndugu Michael Lushinge (Smart), ambaye alisisitiza mshikamanano, mshikamano na ari ya ushindi wa chama katika uchaguzi ujao.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi na wagombea mbalimbali wakiwemo:
- Madiwani wa kata zote 30 za Wilaya ya Kwimba (ambayo ina majimbo mawili: Kwimba na Sumve).
- Moses Bujaga, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Sumve.
- Wagombea Udiwani viti maalum.
- Wagombea Ubunge viti maalum Mkoa wa Mwanza.
- CDE Seth B. Masalu, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mwanza.
- Mhe. Kasalali Mageni, Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumve.
- Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mwanza.
Wananchi walionyesha imani kubwa kwa wagombea wao na kuahidi kushiriki kikamilifu katika kampeni na uchaguzi, kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa wagombea wote wa CCM katika jimbo hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...