Na Said Mwishehe,Michuzi TV- Ruvuma

MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amewapongeza  wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kwa uzalishaji mzuri wa mazao ya biashara na chakula 

Ametoa pongezi hizo leo Septemba 21,2025 alipokuwa katika mkutano wa kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu akiwa Uwanja wa Mbambabay wilayani Nyasa mkoani Ruvuma ambapo ameeleza hatua ambazo Serikali imeendelea kuchukua katika sekta ya kilimo.

Ameeleza miongoni mwa hatua hizo ni serikali imekuwa ikiendelea kufanya jitihada kutafuta bei nzuri ya mazao."Kahawa kwa mfano mpaka mwaka 2022 walikuwa wakiuza sh. 4,500 lakini mpaka jana kahawa inauzwa sh. 12,500 hiyo ni bei ya kahawa kwa kilo. Tutaendelea kuhangaika kutafuta bei nzuri za mazao.

"Mahindi, wakipita walanguzi mnawauzia kwa sh. 450 hadi sh. 500, lakini vituo vyetu vya NFRA vinanunua kilo kwa sh. 700 kwa hiyo niwaomba subiri NFRA mje muuze.”

Pamoja na jitihada hizo, Dk.Samia amesema Serikali pia imekusudia kuimarisha mfumo wa stakabadhi ghalani na masoko ya mazao ya biashara na tutaanzisha vituo vya ukodishaji zana za kilimo."

Kuhusu ajira,Mgombea Urais Dk.Samia  amesema  Ilani ya Uchaguzi (2025 - 2030) serikali imekusudia kujenga viwanda vya kuongeza thamani ya mazao kila wilaya.

Alisema serikali itaanza na wilaya zenye uzalishaji mkubwa ambapo kwa Nyasa utafungwa mtambo wa kukaushia samaki eneo la Mbambabay.

Pia, ameeleza kwamba  serikali itafunga mtambo wa kukoboa kahawa ili kuongeza thamani hatua ambayo itachangia ongezeko la ajira kwa vijana.

Dk. Samia amesema  serikali inakusudia kujenga soko kubwa la kimataifa Mbambabay ambalo litakuza mapato na kuongeza fursa wananchi na kuhudumia nchi za Malawi na Msumbiji."Hata wale wanaovuna dagaa wataweza kupata wateja wengi na bei nzuri.”

Kwa upande wa uvuvi, ameeleza kuwa  serikali imejipanga kuongeza ufugaji samaki katika vizimba kuongeza uzalishaji na fursa kwa wananchi na kuongeza serikali itaendelea kutoa vifaa vya kisasa vya uvuvi ikiwemo kukodisha boti za uvuvi na kupata boti ya uokozi Ziwa Nyasa.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...