Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Mtwara.

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM)Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inakwenda kuongeza matumizi ya teknolojia za kisasa ikiwemo akili unde ili kuimarisha ufanisi katika uzalishaji na utoaji huduma ikiwemo kwenye kilimo.

Dk.Samia ameyasema hayo leo Septemba 25,2025 alipokuwa akihitimisha mkutano wa kampeni katika Mkoa wa Mtwara baada ya kufanya mikutano katika majimbo mbalimbali ya Mkoa huo.

Katika miaka mitano ijayo Serikali inakwenda  kufundisha teknolojia ambayo haitafuta, haitaharibu na haitawapotosha vijana wetu wakakiuka mila na desturi zetu.”

“Kwa kadri inavyowezekana teknolojia tunayokwenda kuitumia tunataka tuirithishe na tuipe hadhi kujenga kizazi kijacho chenye maadili.

“Kwenye kilimo tumeanza sasa kwani tunatafiti tunazozifanya kwa njia za kisasa nazo ni tafiti za mbegu, udongo na tafiti mbalimbali katika kilimo tunazifanya kutumia teknolojia ya kisasa.

“Julai mwaka huu nimefungua maabara kubwa ya kitaalamu ambayo inakwenda kufanyakazi hiyo.Pia mwaka 2024 nilifungua maabara ya kisasa pale sokoine inayokwenda kuwafundisha vijana wetu jinsi ya kuzalisha kitaalamu kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

“Vilevile tunakwenda kutumia zana za kisasa kwenye kilimo na ndiyo maana tunasema tutakuwa na vituo vya zana za kilimo ambapo wakulima wataweza kulima kwa bei nafuu na zana wazitumie. “

Ameongeza kwenye masuala ya vipimo Serikali imeanza kuona kwenye uzalishaji kwa kutumia teknolojia ya kisasa ambapo wale wanaokwenda kuuza NFRA  wakifika pale ni teknolojia inayotumia kutoa unyevu wa mahindi na mizani za kisasa kujua uzito na papo hapo anapata risiti yake kwa mashine hiyohiyo na anapokea meseji kwenye simu yake.

“Kwamba umeleta mzigo fulani, unyevu upo kiasi fulani na gredi ya mazao yako kiasi fulani pesa zako kwa bei ni kiasi fulani.Tunakwenda kutumia teknolojia kwenye kilimo na kwenye mambo mengine yote. Lakini hata kwenye masoko. 

“Minada ya korosho mnashuhudia inavyofanyika watu wapo mbali wanashindana kwa bei tunaona kwenye screen huyo katoa bei fulani.Mbali na kilimo tunakwenda kutumi teknolojia kuimarisha mawasiliano, ufuatiliaji hali ya hewa na mengineyo. 

“Teknolojia hii ndiyo inakwenda kufundishwa mashuleni na vijana wetu wanakwenda kuitumia.Hapa ndipo nakwenda kuunganisha teknolojia ambayo itazingatia mila,tamaduni na desturi.”

Amesisitiza kuwa Serikali inakwenda  kufundisha teknolojia ambayo haitafuta, haitaharibu na haitawapotosha vijana wetu wakakiuka mila na desturi zetu.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...