*Aihitimisha kampeni zake mkoani humo kwa kishindo …wananchi wamuahidi kutiki Oktoba 29


Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Mtwara.

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM amesema katika miaka mitano iliyopita Mkoa wa  Mtwara kwa upande wa huduma za kijamii uwekezaji mkubwa umefanyika kwenye maeneo mbalimbali.

Akizungumza leo Septemba 25,2025 katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Sabasaba uliopo Mtwara Mjini mkoani Mtwara Dk.Samia ametumia nafasi hiyo kuelezea hatua za maendeleo ambazo Serikali imezifanya ndani ya Mkoa huo.  

"Kimkoa nakumbuka Septemba 15, 2023 nilikuja kuzindua hospitali ya rufaa kanda ya kusini ambayo imesogeza huduma za kibingwa karibu zaidi na wakazi wa Mtwara, Lindi na Ruvuma.

"Mbali na hospitali hiyo, Mkoa wa Mtwara sasa una hospitali mbili za rufaa ambayo ya Ligula na Ndanda. Pia kuna hospitali tatu za halmashauri (Manispaa ya Mtwara, Nanyamba na Wilaya ya Mtwara) haya ni maendeleo ndugu zangu," alisisitiza.

Amewaahidi wananchi wa mkoa huo kwamba serikali yake itaboresha zaidi huduma zinazotolewa kwa kupeleka vifaa tiba zaidi na kuongeza watumishi wa afya.

Katika hatua nyingine, Mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema serikali ilishapeleka fedha Sh.bilioni 87 kwa ajili ya miradi ya maji huku akieleza iwapo atapewa  ridhaa ya kuliongoza taifa atakwenda kukamilisha mradi uliobaki wa Makonde kutoa maji kutoka Mto Ruvuma.

Amesema kwamba mradi huo utamaliza changamoto ya uhaba wa maji Nanyamba, Mtwara Mjini na vijijini.Lengo la Serikali baada ya miaka mitano kukamilika kila Mtanzania apate huduma ya maji safi na salama.

"Miradi midogo ambayo ipo maeneo mbalimbali nayo tunakwenda kuikamilisha. Pia tunafanya uwekezaji huu kwenye elimu sawa kwamba tunapanda mbegu sasa hivi na mazao yake tutakuja kuyavuna miaka ya baadaye ijayo.

"Hii ni mbegu tunataka watoto wasome kwenye mazingira mazuri siyo yale tuliyosomea sisi. Wawe na vifaa vyote vya kujifundishia na vya kufunziwa. Walimu wawe na vifaa vyote.

Aidha amesema mpango wa Serikali ni kuona kuna mazingira mazuri ya elimu katika ngazi zote na kuwe  na wasomi wazuri ili kujanga kesho iliyobora kwa Tanzania yetu."

Dk.Samia pia amesema anatambua licha ya kazi nzuri inayofanyika, bado kuna uhaba wa walimu, nyumba za walimu kazi ambayo CCM imeahidi kwenda kuifanya ikipewa ridhaa.

Pamoja na hayo amewahakikishia wananchi hao kuwa kitaifa miaka mitano ijayo itakuwa miaka ya kupiga hatua kubwa katika matumizi ya teknolojia ya kisasa na vilevile miaka mitano ijayo Serikali inataka kuchukua hatua za makusudi kudumisha mila, tamaduni na desturi zetu siyo zile zenye madhara.

Kwa upande wa wananchi wa Mkoa wa Mtwara ambao wamezungumza na Michuzi Blog baada ya Mgombea Urais Dk.Samia akihitimisha kampeni zoke katika Mkoa huo wamesema wamekuwa wakifuatilia mikutano yake tangu slippingia kwenye Mkoa huo na maendeleo ambayo ameyafanya yamegusa wananchi wote.

“Kwa Mkoa wa Mtwara tunajivunia uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na hasa katika kutoa Mbolea na salfa bure kwa wakulima wa korosho amegusa maisha yetu.

“Katka huduma za kijamii Mtwara imepiga hatua kubwa za maendeleo.Ahadi yetu kwake Oktoba 29 mwaka huu tunakwenda kumpigia kura ya heshima na tutahakikishia tunaongoza kwa kumpigia kura nyinyi ili ashinde kwa kishindo.”









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...