Na Said Mwishehe,Michuzi TV -Pwani.

KATIKA kukabiliana na changamoto ya uhaba wa maji katika Mkoa wa Pwani ,Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imetoa fedha Sh.bilioni 187.3 katika mkoa huu. Uwekezaji huu umewezesha kuimarisha hali ya upatikanaji maji safi na salama kutoka asilimia 67 hadi asilimia 89.

Akizungumza leo Septemba 28,2025 mbele ya maelfu ya wananchi wa Kibaha mkoani Pwani mgombea Urais Dk.Samia amesema anatambua bado kuna maeneo ambayo bado upatikanaji maji haujawa mzuri lakini kazi inaendelea. 

“Tunapoenda mbele tutakamilisha miradi mingine minne yenye thamani ya sh. bilioni 44.Miradi  hiyo imeshaanza kutekelezwa itakayohudumia kata 53 za Wilaya ya Rufiji, Kibiti Mkuranga na Kisarawe.

Pia, amesema  mradi wa maji Kwala utakaonufaisha maeneo ya Kwala, Bandari Kavu na maeneo ya viwanda wakati mradi wa maji Pangani utatatua changamoto ya maji Kata Pangani pamoja na maeneo ya Msufini, Lulanzi na TAMCO.

Ameongeza kuwa mbali na miradi hiyo miradi mingine midogo yenye kuhusisha upanuzi wa mtandao wa maji kutoka Mlandizi, Bokomlegela, Janga, Mtongani na Kawawa itatekelezwa.

Akieleza kuhusu changamoto amesema  serikali itajenga mradi wa maji katika eneo la viwanda wenye gharama ya sh. bilioni 10.9 utanifaisha maeneo ya mbalimbali ya mkoa huo.

Kuhusu afya Dk.Samia amesema  serikali imefanya maboresho makubwa katika Hospitali ya Tumbi ambayo yamehusisha kuanzisha kituo cha kusafisha damu.

"Tumeleta vifaa tiba vikiwemo CT Scan, X Ray na Utra Sound vyote vimesogeza huduma muhimu karibu zaidi na wananchi. Vipimo vyote sasa vinapatikana Tumbi.Tunafikiria kuweka MRI ili vipimo vyote vipatikane pale na wananchi wapate huduma bora zaidi.”

Pia amesema serikali imeongeza vijiji vyenye miundombinu ya umeme kutoka vijiji 282 mwaka 2020 na sasa vijiji vyote 415 vimepata umeme.Kazi inayoendelea ni kuunganisha katika vitongoji ambapo kazi hiyo imeshafanyika katika vitongoji mbalimbali.

Akizungumzia umeme amesema Serikali  imekamilisha ujenzi wa kituo kipya cha umeme katika mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere kisha kuunganisha katika gridi ya taifa.

"Tunajenga njia mpya ya umeme katika kituo cha Chalinze lakini tunajenga njia mpya ya umeme ya Kv 400 kutoka Chalinze - Kinyerezi hadi Mkuranga. Hivyo niwahakikishie kuwa tunakwenda kuwa na umeme wa uhakika tukikamilisha miradi hii ya umeme.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...