Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Chalinze

SERIKALI tutampa zawadi maalum Rais Mstaafu Jakaya Kikwete! Hivyo ndivyo ambavyo mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ameeleza wakati akieleza mpango wa Ujenzi wa Uwanja mkubwa na wa kisasa wa michezo eneo la Msoga mkoani Pwani.

Akizungumza na wananchi wa eneo la Chalinze mkoani Pwani akiwa katika mkutano wa kampeni Dk.Samia amesema mpango wa Serikali kujenga Uwanja huo kutambua mchango wa Rais Mstaafu katika Serikali ya Awamu ya Nne Jakaya Kikwete.

"Serikali inajipanga kujenga uwanja mkubwa wa michezo Msoga na hii ni shukrani yetu kwa utumishi wa Rais wa Awamu ya Nne. 

"Mengi tumeyapa majina yake lakini kwa Msoga hatujafanya kitu. Kwa hiyo uwanja ule tunakuja kuujenga Msoga kuonyesha shukrani yetu kwa Rais wa Awamu ya Nne.

Alisisitiza: "Kwa hiyo wanachalinze mtakuwa na uwanja mkubwa wa michezo pale msoga,”amesema Dk.Samia ambaye leo amefanya mkutano mkubwa na midogo akiwa katika Mkoa wa Pwani. 

Kwa kukumbusha tu Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ni mzaliwa na mkazi wa eneo hilo la Msoga ambako hata baada ya kustaafu nafasi ya Urais ameamua kuweka kambi ya kudumu Msoga ambako ndiko yalipo makazi yake.

Pia Kikwete ni moja ya viongozi ambaye amekuwa na mahaba ya kweli na sekta ya michezo nchini na katika utawala wake alichukua hatua mbalimbali za kuhakikisha michezo inapewa nafasi kubwa zaidi.”













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...