Na Said Mwishehe,Dodoma
MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rais Dk.Samia Suhusu Hassan amepokelewa na maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma huku akitumia nafasi hiyo kuwaeleza wana Bahi kwamba yajayo yanafurahisha.
Akizungumza mapema leo Septemba 9,2025 na wananchi wa Wilaya ya Bahi akitokea Dodoma kuelekea mkoani Singida Dk.Samia Suluhu Hassan amepata nafasi ya kusimama na kuomba kura kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.
“Mbele tunakokwenda yanakuja makubwa zaidi na wanasema yajayo yanafurahisha na dhamira yangu ni kuona katika miaka mitano ijayo inayokuja tunafanya mambo makubwa zaidi.
Dk.Samia Suluhu Hassan amesema kwa upande wa mafanikio amesema wameboresha huduma za afya kwa kutekeleza miradi mbalimbali inayogusa maisha ya wananchi.
“Tumejenga Hospitali ya Wilaya lakini vizur tumejenga vituo vya afya na zahanati. Sasa huduma za afya zinaendelea najua hatujamaliza kila mahali lakini kasi itaendelea huduma za afya kwa wananchi zitaendelea.
“Kwa upande wa elimu tumejenge shule msingi 14 na kufanya kuwa na jumla 86.Tumejenga shule tatu za sekondari na sasa zipo 25 mbali na hayo tunafikiria kujenga mabweni kwa watoto wa kike.Kwa sababu tumeona mwenendo wa watoto wa kike na destuli zetu zinawazuia watoto wa kike kwa hiyo tubafikiria kuwajengea mabweni. “
Akieleza zaidi ambayo Serikali imetekelezwa kwa Wilaya ya Bahi ,Mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na hayo wamejenga vyuo vya VETA viwilli ambako kuna wanafunzi 156 ambao wanaendelea na mafunzo ya fani l mbalimbali za ujenzi ushoni,kompyuta, ufundi umeme wa magari na majumbani na magari.
“Na hizi ndizo fani ambazo kazi zake zitakazowatoa vijana wetu kwa sababu wapo mijini na njia kubwa. Tutafikiria baadae kuwa na fani ya kilimo na ufugaji,”amesema Dk.Samia.
Kuhusu sekta ya kilimo Rais Dk.Samia ha mgombea Urais amesema wameshakarabati skimu na ukarabati unaendelea hivyo wakulima watalima mara mbili kwa mwaka.
Kwa upande wa maji amesema wameongeza miradi kadhaa ya uchimbaji visima na sasa vijiji 56 kati ya 59 vinapata huduma ya maji. “Najua bado mahitaji ya maji ni makubwa hasa kwenye vijiji Mpamantwa na Ipima.Kuna Mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria kupitia Singida hadi Dodoma, hivyo na Bahi watapata maji kupitia bomba la maji litakalopita.
“Na hilo ndilo kusudio letu na siyo kwa matumizi tu ya majumbani peke yake lakini pia na kilimo. Lakini katika maji kitaifa tumefanya vizuri, maeneo mengi Tanzania yanahitaji maji lakini kazi inaendelea lakini tutahakikisha tunapokwenda mbele kila mtanzania anapata maji safi na salama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...