*Mwingine anasema atatoa elimu bure…kwani CCM hatujatoa ?
Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Lindi
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema kwamba hakuna chama kitakachoweza kwa sasa hivi kulinda na kuinua utu wa Mtanzania kama kama Chama hicho.
Dk.Samia ametoa kauli hiyo leo Septemba 25,2025 alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi wa Jimbo la Mchinga mkoani Lindi ambako ameendelea na mkutano wa kuomba kura kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.
“Na ndiyo maana tumekuja na hii kauli mbiu ya kazi na utu. Maana yake tupeni ridhaa yenu Chama Cha Mapinduzi tuendeshe nchi hii tena kwa miaka mitano ijayo.
“Huko mbele tutakuja tena kutufanyia tathmini, tufanye kazi ili tuinue utu wa mtanzania na katika kuinua utu wa mtanzania ni kumpatia maji safi na salama, elimu, huduma za afya, umeme, kilimo, huo ndiyo kulinda na kuukuza utu wa mtu.
“Chama Cha Mapinduzi ukisoma ilani yetu yote utaona tunakwenda kufanyakazi ya kukuza na kuulinda utu wa mtanzania tu wa mwananchi,”amesema Dk.Samia mbele ya wananchi hao wakiongozwa na mgombea ubunge wa Jimbo la Mchinga Salma Kikwete.
Dk.Samia amesema pia kuna wengine wanapitia ilani yao kwa wanadokoa dokoa. “Wanasema tutatoa elimu bure kwani CCM haijatoa? Tunatoa msingi mpaka kidato cha sita. Lakini kuna fungu la mkopo ukienda chuo kikuu tunakwambia kopa hapa kijana kasome ukipata kazi ukijiajiri utarudisha polepole.
“Mwingine anakwambieni nitaleta maji, alikuwa wapi asilete siku zote. CCM tumeshaleta maji. Kwa hiyo ahadi zao ni za kuigiza tu. Niwaombe sana wananchi tarehe 29 mwezi wa 10 nendeni mkachague chama cha mapinduzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...