*Asema zitawaka kwa saa 24 ili kutoa fursa wananchi kufanya biashara muda wote
Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Tabora
MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu Dk.Samia Suluhu Hassan amehutubia maelfu ya wananchi Mkoa wa Tabora huku akiahidi maendeleo zaidi ikiwemo ujenzi wa barabara ya mzunguko, taa za barabarani na madaraja.
Akizungumza na maelfu ya wananchi wa
mkoa wa Tabora leo Septemba 12,2025 katika Uwanja wa Nanenane Ipuli mkoani hapa Dk.Samia Suluhu Hassan amesema katika miaka mitano ijayo Serikali imepanga kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya barabara za mijini na vijijini katika mkoa huo.
Dk.Samia aliyetumua mkutano kueleza maendeleo yaliyopatikana katika Mkoa wa Tabora amesema kitaifa miundombinu hiyo iliimarishwa kwa kuongeza bajeti ya Tarura kwa mwaka huu wa fedha kutoka sh. bilioni 700 hadi sh. trilioni 1.9 ili kufungua barabara vijijini na kujenga za mijini.
Pia amesema kuwa barabara za changarawe zimejengwa maeneo mbalimbali ambazo zitapitika kwa mwaka mzima.
"Kwa hapa Tabora Manispaa nina furaha kuwajulisha tunakuja na ujenzi wa barabara mpya ya mzunguko ya Tabora mji, tumeshaifanyia tathmini itakayokuwa na urefu wa kilometa 82.Ili kuhakikisha magari yote yasiyokuwa na ulazima kupita ndani ya mji wa Tabora, yapite katika barabara hiyo ya nje kwenda yanayoelekea.”
Ameeleza kuwa anataka Tabora yenye historia kubwa iwe na hadhi kubwa pia huku akieleza katika hatua nyingine ndani ya Mkoa wa Tabora Serikali katika miaka mitano inakwenda kujenga madaraja 133.
“Madaraja hayo yatajengwa katika barabara zilizojumuishwa katika Ilani ya uchaguzi ambazo zinakwenda kujengwa.Pia serikali itakwenda kujenga taa za barabarani 2,500 hivyo mkoa huo na wilaya zake zitapata fursa kufanyabiashara saa 24.
"Kwa sababu umeme ni usalama, umeme ni mwanga. Umeme unasaidia katika uzalishaji, hivyo tunakwenda kuweka mataa ili vijana wapate fursa kufanyabiashara saa 24.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...