Morogoro,

Baadhi ya Walipakodi mkoani Morogoro wameeleza kuvutiwa na elimu ya kodi mlango kwa mlango inayotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kueleza namna linavyowasaidia kutatua changamoto zinazowakabili wakiwa katika maeneo yao ya biashara.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walipotembelewa na timu ya kutoa elimu ya kodi mlango kwa mlango mkoani morogoro iliyongozwa na Meneja wa TRA mkoani humo Bw. Sylver Rutagwelera baadhi ya wafanyabishara hao akiwemo Bi. Sprian John na Zainudin Yaman wameshauri elimu hiyo iwe endelevu.

Wamesema kupitia zoezi hilo la elimu ya mlango kwa mlango wafanyabiashara ambao hawalipi kodi nao wataanza kulipa kodi na kuongeza idadi ya walipakodi hali ambayo pia itaongeza mapato ya Serikali.

Wameeleza kuwa katika siku za karibuni kumekuwa na ukaribu baina yao na TRA hali ambayo imewawezesha kuelewa umuhimu wa kulipa kodi na kutimiza wajibu huo kwa wakati bila kuvutana na TRA.

“Uongozi wa TRA mkoani kwetu umekuwa ukitutembelea mara kwa mara ili kuona mwenendo wa biashara zetu na kutusikiliza, tunawashukuru na kuwapongeza maana hawakai ofisini hasa huyu meneja amekuwa karibu sana na wafanyabiashara” amesema Zainudin Yaman.

Walipakodi hao wamewashauri wafanyabiashara wengine ambao wamekuwa wakikwepa kodi na kutokutoa risiti kubadilika kwa faida ya nchi na biashara zao kwa ujumla.

Kwa upande wake Meneja wa TRA mkoa wa Morogoro Bw. Sylver Rutagwelera amewashukuru na kuwapongeza Walipakodi mkoani humo kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari na kueleza kuwa TRA imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha kwamba inatatua changamoto zinazowakabili.

Amesema katika zoezi la kutoa elimu ya kodi mlango kwa mlango wameweza kuwafikia wafanyabiashara wengi na kuongeza wigo wa kodi na idadi ya walipakodi kutokana na kubaini kuwepo kwa walipakodi wengi ambao walikuwa bado hawajasajiliwa na kuanza kulipa kodi.

“Kupitia zoezi hili wafanyabiashara wengi wamefikiwa kusikilizwa na kutatuliwa changamoto zao ambapo pia tumeweza kuwasajili wafanyabiashara ambao walikuwa hawajasajiliwa na kuanza kulipa kodi, hali ambayo itaongeza pia makusanyo ya kodi mkoani kwetu” amesema Bw. Rutagwelera.

Ameeleza kuwa zoezi hilo la elimu ya mlango kwa mlango litafanyika katika wilaya zote za mkoa wa Morogoro.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...