SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza jumla ya tani 50 za bidhaa hafifu zenye thamani ya shilingi milioni 525, ambapo kati ya hizo tani 40 zimeisha muda wake wa matumizi.
Zoezi hilo la uteketezaji limefanyika leo katika dampo la Pugu, jijini Dar es Salaam,
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Meneja wa TBS Kanda ya Mashariki, Bi. Noor Meghji, alisema bidhaa hizo zilipatikana kupitia ukaguzi uliofanyika katika maeneo ya Ifakara, Mlimba na Manispaa ya Morogoro, mkoani Morogoro; Chalinze, Bagamoyo na Kisarawe, mkoani Pwani; pamoja na manispaa zote za Dar es Salaam.
Amezitaja bidhaa zilizokamatwa kuwa ni bidhaa za chakula ambazo hazikidhi viwango, ikiwemo maziwa ya watoto (baby formula), soda, vinywaji vya kusisimua mwili (energy drinks), pamoja na bidhaa zilizokwisha muda wa matumizi zikiwemo cornflakes na nyanya zilizokaangwa (tomato paste).
“Tunawataka wafanyabiashara wa jumla kuacha tabia ya kuwauzia wafanyabiashara wa rejareja bidhaa zilizopitwa na muda wa matumizi kwa lengo la kuondoa bidhaa hizo sokoni, kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha afya za wananchi,” amesema Bi. Meghji.
Aidha, amewataka walaji kuwa makini kwa kuhakikisha bidhaa wanazonunua zinakidhi matakwa ya ubora kwa kuangalia tarehe ya mwisho wa matumizi pamoja na alama ya ubora.
“Suala la usalama wa chakula ni mtambuka, kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa, kusambazwa na kuuzwa sokoni zinakuwa salama. Walaji wanapaswa kujiridhisha kabla ya kutumia bidhaa yoyote,” amesisitiza.
Kwa mujibu wa TBS, operesheni za ukaguzi na uteketezaji wa bidhaa zisizokidhi viwango zitaendelea nchi nzima ili kulinda afya za wananchi na kudhibiti biashara haramu ya bidhaa hafifu sokoni.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...