Na Tobietha Makafu & Janeth Mesomapya
Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetembelea mradi wa kuzalisha umeme kwa nishati ya jua uliopo Kishapu, mkoani Shinyanga, leo tarehe 27 Septemba 2025.
Akitoa taarifa kwa Bodi, Meneja wa Mradi Mha. Emmanuel Anderson alisema, mradi huo unatekelezwa kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza itakayozalisha Megawati 50, imefikia asilimia 78.1, itakamilika Desemba 2025.
Awamu ya pili itakayozalisha MegaWati 100, itaanza Februari 2026 na kukamilika kwake kutaongeza uzalishaji kwa megawati 100 zaidi ambazo zitaingizwa katika gridi ya taifa.
“lengo la mradi huu ni kutekeleza malengo ya taifa kuongeza uzalishaji wa nishati jadidifu, kuongeza upatikanaji wa umeme wa bei nafuu na rafiki wa mazingira, kuboresha msongo wa umeme katika eneo la Kanda ya Ziwa na kupunguza utegemezi wa nishati inayotumia mafuta/gesi kwa kutumia nishati safi” aliongeza Mha. Anderson.
Naye Mjumbe wa Bodi na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati, Eng. Ngosi Mwihava, alisema lengo la ziara hiyo ni kujionea hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo. Alisema kwa kuwa EWURA ndiyo Mamlaka yenye jukumu la kutoa leseni ya uzalishaji, ni muhimu kwa Bodi kuwa na uelewa mpana kuhusu mwenendo wa utekelezaji wa mradi ili iweze pia kutoa ushauri pale utakapohitajika.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mheshimiwa Peter Masindi, alisema mradi huo umeendelea kutoa fursa kwa Watanzania kwani takribani asilimia 95 ya wafanyakazi waliopo ni wazawa. Pia alieleza kuwa miradi ya uwajibikaji kwa jamii (CSR) ipo kwenye hatua za maandalizi ili kuhakikisha jamii inayozunguka inanufaika moja kwa moja.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...