HaloPesa, huduma ya kifedha ya Halotel, Leo imezindua rasmi kampeni mpya iitwayo “Tamba na Bonasi”, sambamba na utambulisho wa msaidizi wa kidigitali anayejulikana kama Mr. Bonasi, ambaye atakuwa kiwakilishi rasmi wa kampeni hiyo.

Kupitia kampeni hii, wateja wa HaloPesa watapata nafasi ya kujishindia bonasi kabambe na kuingia kwenye droo za kila siku, kila wiki, na kila mwezi kwa kufanya miamala mbalimbali kupitia HaloPesa, ikiwa ni pamoja na kutuma pesa, kutoa pesa, Malipo ya bili na bidhaa, kununua umeme (LUKU) nk...Wateja watajipatia nafasi ya kushinda hadi Shilingi Milioni Mbili (Tsh 2,000,000) pesa taslimu.

Mbali na hivyo HaloPesa inawapa urahisi wateja wanapofanya miamala HaloPesa kwenda HaloPesa ni bure bila makato kupitia HaloPesa App, lakini pia kununua Luku kupitia HaloPesa App ni bure. ni mwendo wa kuserereka tu!

Akizindua kampeni hiyo, Mkuu wa Idara ya Biashara HaloPesa, Bi Happy Mzena, alisema:

"Uzinduzi huu ni sehemu ya mkakati wetu wa kuendelea kutoa thamani zaidi kwa wateja wetu. Mr. Bonasi siyo tu nembo ya kampeni hii bali ni jukwaa la kidigitali la zawadi, linaloleta msisimko katika kila muamala. Lengo letu ni kuifanya kila huduma ya HaloPesa kuwa fursa kwa wateja wetu”.

"Tunatoa wito Kwa wateja wetu wote waendelee kufanya miamala kupitia HaloPesa, iki waweze kutamba zaidi na bonasi na huenda ukawa mshindi wa zawadi kubwa kutoka kwa Mr. Bonasi."

Kwa upande wake, Afisa Masoko wa HaloPesa, Bi. Aidat Lwiza, alieleza Kwa kina ubunifu na thamani ya kampeni hiyo kwa wateja:

“‘Tamba na Bonasi’ ni uzoefu wa kipekee wa kidigitali uliobuniwa kwa ajili ya wateja wetu wa HaloPesa. Mr. Bonasi amekuja kuleta msisimko mpya, akiwaletea wateja zawadi kwa njia ya kipekee, rahisi na ya kuvutia. Kupitia teknolojia ya kisasa, wateja wetu sasa wanaweza kujishindia kila wanapofanya miamala ya kila siku."

“Tunaamini kuwa huduma za kifedha hazipaswi kuwa tu rahisi na salama, bali pia ziwe na mvuto, thamani ya nyongeza, na zawadi. HaloPesa imeendelea kuwa kinara sokoni kwa kutoa makato nafuu zaidi ukilinganisha na huduma nyingine, huku ikijivunia kuwa na huduma bora kwa wateja nchi nzima. Tuna mtandao mpana wa mawakala na maduka ya Halotel kote nchini, kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bila usumbufu.”

“Zaidi ya yote, kupitia kampeni hii, maelfu ya wateja wanapata nafasi ya kujishindia na kushine na Mr. Bonasi – kila siku, kila wiki na kila mwezi. Tunawakaribisha Watanzania wote kujiunga na HaloPesa, kwa sababu sasa, kila muamala sio tu njia ya kutuma au kupokea fedha, bali ni hatua moja kuelekea ushindi halisi.”

Bi. Aidat aliendelea kuhimiza umuhimu wa usalama wa taarifa binafsi kwa wateja wakati wa kampeni hii:

“Taarifa zote za ushindi zitatumwa kupitia ujumbe rasmi wenye jina la ‘HaloPesa’ tu! na simu zozote kutoka kwetu zitatoka kupitia namba ya huduma kwa wateja 100. Tunawakumbusha wateja wetu kuwa waangalifu, wasitoe taarifa binafsi kwa namba au watu wasiothibitishwa. Kwa msaada zaidi, tafadhali tembelea maduka yetu au piga simu bure kupitia 100.”












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...