NA MWANDISHI WETU,IRINGA


Katibu Mkuu wa umoja wa wanawake (UWT) Taifa Ndg. Suzan Peter Kunambi (MNEC) amewahimiza wanawake kuweka misingi imara ya kuwa na umoja na mshikamano hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Octoba 29 mwaka huu.

Katibu huyo ameyasema hayo wakati wa mikutano mbali mbali kwa ajili ya kuweza kuwanadi na kuwaombea kura wagombea wa CCM katika nafasi ya Urais,Ubunge pamoja na udiwani.

"Kitu kikubwa nawaomba wanawake wenzangu wa iringa mjini pamoja na iringa vijijini kuhakikisha mnashikamana kwa pamoja ili tuweze kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaks huu,"amebainisha Katibu huyo.

Aidha Katibu huyo kupitia mikutano hiyo ameweza kupata fursa ya kuwapokea wanachama wapya 7 kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Baadhi ya wanachama hao ambao wamejiunga na CCM wameahidi kuungana na wanachama wa CCM katika kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa UWT Suzan Peter Kunambi amemnadi wagombea wa CCM nafasi ya Udiwani kata ya Migori Ndg. Fatma Moge, huku akiwaomba wananchi kumchagua kwa kura nyingi za kishindo Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pia katibu huyo amewaomba wana ccm kumpa ridhaa ya kuwaongoza na kumpa kura nyingi Ndg.William Lukuvi ambaye ni Mgombea wa Ubunge Jimbo la Isimani Wilaya ya Iringa Vijijini.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...