• Suluhisho maalumu za kifedha kuwawezesha wahandisi, mafundi na wafanyakazi wa mgodi kujenga mali, kumiliki makazi na kulinda mustakabali wa familia zao.
Geita, Tanzania – Ijumaa, 12 Septemba 2025:
Geita ni kiini chaa sekta ya madini nchini Tanzania, ukiwa makazi ya maelfu ya wanaume na wanawake wanaochangia kwa bidii ukuaji wa uchumi wa taifa. Kwa kutambua mchango na ndoto zao, Benki ya Stanbic Tanzania imetangaza kujidhatiti katika kuwawezesha wafanyakazi wa migodini Geita kupitia suluhisho bora za kifedha zinazowawezesha kustawi, kuwekeza na kujenga mustakabali wa kudumu.
Tangazo hili lilitolewa wakati wa hafla maalumu ya wafanyakazi wa migodini, ambapo Stanbic ilitambulisha rasmi suluhisho za mikopo ya nyumba, mikopo binafsi, huduma za akiba na uwekezaji zilizobuniwa mahsusi kulingana na uhalisia wa maisha ya wafanyakazi wa sekta ya madini.
“Geita siyo tu kitovu cha madini, ni jamii ya watu wenye maono makubwa wanaoendesha gurudumu la uchumi wa Tanzania,” alisema Emmanuel Mahodanga, Mkuu wa Kitengo cha wateja Binafsi (Personal Banking) Stanbic Tanzania. “Benki ya Stanbic tunaamini wafanyakazi hawa wanastahili suluhisho za kifedha zinazolingana na malengo yao. Iwe ni kumiliki nyumba, kujenga utajiri au kulinda familia zao, tupo bega kwa bega kuhakikisha ndoto hizo zinatimia.”
Miongoni mwa huduma zilizotambulishwa ni mikopo ya nyumba yenye thamani ya hadi TZS bilioni 1.2 yenye muda wa marejesho wa hadi miaka 20, inayowawezesha wafanyakazi wa migodini kumiliki makazi bora. Stanbic pia imetambulisha mikopo ya moja kwa moja ya ununuzi wa nyumba (straight purchase loans) ambapo benki inagharamia hadi 90% ya thamani ya nyumba, huku mteja akichangia 10% pekee, pamoja na nafasi za kuhamisha mikopo ya nyumba (takeover mortgages) kwa masharti nafuu zaidi.
Kwa wale wanaohitaji kuboresha maisha yao na kuongeza tija kazini, huduma za mikopo ya magari na vifaa pia zimeangaziwa, ikihusisha magari binafsi, mabasi, hadi vifaa vya migodini kama vile excavators, bulldozers na drilling rigs.
“Wafanyakazi wa migodini wanastahili kuwa na nyenzo zinazorahisisha maisha yao na kuongeza ufanisi wa kazi. Kupitia masharti rahisi ya marejesho, tunawapa fursa hiyo,” alisema Herry Magava, Meneja wa Mikopo ya Magari na Vifaa (Vehicle and Asset Finance) Stanbic Tanzania.
Zaidi ya mikopo, Stanbic pia imetambulisha mikopo ya ujenzi wa nyumba, fursa za akiba na uwekezaji, pamoja na bima ya mikopo (credit life insurance), ikihakikisha wafanyakazi hawajengi tu mali, bali pia wanalinda familia zao dhidi ya changamoto za ghafla.
Hatua hii ni sehemu ya safari ya miaka 30 ya Stanbic nchini Tanzania chini ya kaulimbiu “Tanzania Mabegani – Miaka 30 ya Kukua Pamoja.” Kwa kuweka mahitaji ya watu binafsi katikati ya huduma zake, benki inaendelea kuthibitisha nafasi yake kama mshirika wa ustawi wa kifamilia, maendeleo ya jamii na mageuzi ya kiuchumi nchini.
“Mwelekeo wetu ni wazi, tupo hapa kuendesha ukuaji wa Tanzania kwa kuwawezesha watu wake. Wafanyakazi wa migodini Geita ni nguzo ya ukuaji huo, na tunajivunia kutembea nao katika safari hii, tukiwawezesha kufikiria makubwa na kufanikisha malengo yao,” alihitimisha Mahodanga.

Afisa Uwekezaji kwa Wateja Binafsi Stanbic Bank,Richi Ndisi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...