Na. Mwandishi wetu,
KITUO cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA) kimekemea vikali tabia za baadhi ya vyama vya siasa kuwalazimisha wananchi kususia uchaguzi ni kuwanyima haki ya msingi kwa mujibu wa katiba.
Chama husika hakishiriki uchaguzi hatua hiyo ambapo ni kinyume cha demokrasia ya kutaka kufanya jaribio la kupora haki za wananchi.
Mwenyekiti wa MECIRA, Mchange Habibu, akizungumza leo katika kipindi cha Kipindi cha Wasafi Good Morning amesema kwa kusisitiza kuwa Demokrasia inasimama juu ya misingi ya uhuru wa mtu mmoja mmoja kufanya maamuzi kwa hiari yake.
“Kila raia ana haki ya kushiriki au kutoshiriki uchaguzi kwa hiari yake. Hii ni haki ya kikatiba isiyoweza kufutwa na chama chochote. Chama kinaweza kususia, lakini haki ya wananchi kushiriki inabaki palepale. Demokrasia halisi inajengwa kwa hoja na heshima, si kwa shinikizo,” alisema.
Amesema wito wa MECIRA kwa Wananchi ni kuhamasisha wananchi wasikubali kulazimishwa juu ya kutopiga kura kwani ni haki yao ya kikatiba na sehemu ya maamuzi ya kuliendea jambo hilo la kupiga kura
Amesema kila kura ni inayipigwa na mwananchi ni sauti yake katika kuja kudai maendeleo kwa kiongozi aliyemchagua na sio mtu ambaye alisusia uchaguzi.
Mchange amesema demokrasia ni uhuru na siyo amri ya kushinikizwa na chama cha siasa ambacho hakijashiriki uchaguzi .
MECIRA imeongeza kuwa mfumo wa vyama vingi unalindwa na Katiba, hivyo hata chama kimoja kisiposhiriki, vyama vingine vinabaki na nafasi ya kushindana kwa mujibu wa sheria.
“Kususia ni mtazamo wa chama fulani, lakini kuwalazimisha raia wote kufuata msimamo huo ni kuua roho ya demokrasia. Kura yako ni thamani yako,” amesema Mchange.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...