Na Munir Shemweta, WANMM ARUSHA
aafisa Mipangomiji wa mikoa ili kujipanga kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
Kikao hicho cha siku tatu kinachofanyika mkoani Arusha kuanzia Sept 01.09.2025 hadi 03.09.2025 kinatumika kukumbushana maadili kwa Maafisa Mipangomiji, muongozo wa upangaji na utekelezaji mipango ya uendelezaji miji, umuhimu wa kufanya ukaguzi wa matumizi ya ardhi pamoja na uidhinishwaji kazi za mipango miji kwenye mfumo wa e-ardhi.
Idara ya Maendeleo ya Makazi moja ya majukumu yake ni kupanga miji vizuri pamoja na kusimamia uendelezaji wake (Development control).
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Deogratias Kalimenze amewaambia washiriki wakati wa kufungua kikao hicho kuwa, Maafisa Mipangomiji ndiyo waliobeba dhamana nzito ya kuhakikisha ulimwengu unakuwa na sehemu salama ya kuishi.
‘’Tumepewa dhamana ya kuhakikisha kwamba tunawafanya watu waishi katika mazingira ambayo ni mazuri, ni mipango yetu ndiyo inayoongoza namna gani watu wataishi, watafanya kazi, ajira zitakavyopatikana, tutalindaje rasilimali zitumike kizazi na kizazi, nishati itumikeje’’ amesema Kalimenze
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa idara ya Maendeleo ya Makazi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, upangaji wa miji ni jukumu ambalo watendaji hao wamepangiwa na mwenyezi mungu waweze kuilinda dunia na kuwa endelevu.
‘’Jukumu mlilokuwa nalo Maafisa Mipangomiji nchini ni kubwa na katika kulitekeleza hilo ni lazima muwe na weledi wa hali ya juu, nidhamu katika kutekeleza majukumu pamoja na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kwa ajili ya kuongoza utekelezaji majukumu ya kila siku ili msisababishe ajali kwa wale mliopewa majukumu ya kuwafanya waishi katika dunia kwa furaha.
Kupitia kikao hicho, tathmini ya utekelezaji wa Bajeti kwa Mwaka 2024/2025 pamoja na utekelezaji kazi za urasimishaji nchini itafanyika. Aidha, kutakuwa na uwasilishaji mada kuhusiana na mfumo wa utoaji huduma za Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipangomiji, kupitia na kujadili rasimu ya kanuni ya viwango vya upangaji na makundi ya matumizi pamoja na namna ya kulinda afya ya akili na umuhimu wa akili hisia katika maeneo ya kazi.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Deogratias Kalimenze akizungumza na Maafisa Mipangomiji wa Wizara kutoka ofisi za mikoa wakati wa kikao kazi kinachoendelea mkoani Arusha tarehe 01.09. 2025.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Deogratias Kalimenze (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Mipangomiji wa mikoa wanaohudhuria kikao kazi cha Maafisa Mipangomiji wa mikoa mkoani Arusha tarehe 01.09.2025. Wa pili kulia waliokaa ni Bi. Desdreia Haule, Afisa Maadili Mkuu kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...