Na Maandishi wetu, Mirerani
KAZAMOYO English Medium pre & primary school iliyopo mtaa wa Kazamoyo Kata ya Endiamtu Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, imeadhimisha mahafali ya 12 ya kuhitimu darasa la saba.

Mkurugenzi wa shule hiyo Samwel Mghamba, ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya 12 ya mahafali ya kuhitimu darasa la saba yaliyofanyika shuleni hapo.

Mkurugenzi Mghamba amesema wanafunzi 32 kati ya 35 walioanza darasa la kwanza mwaka 2019 wamefanikiwa kuhitimu darasa la saba.

Mghamba amesema tangu waanze muhula mpya wa masomo mwanzoni mwa mwaka 2025 uongozi wa shule umejiwekea malengo mbalimbali.

Ametaja malengo hayo ni kiwango cha ufaulu kinabaki wastani wa A na kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji, uboreshaji wa majengo, ununuzi wa samani na uboreshaji wa mandhari ya shule kwa jumla.

"Umaliziaji wa jengo la kompyuta lenye vyumba viwili lililofikifia hatua ya mtambaa panya lililobakiza shilingi milioni 20 kukamilika na kukarabati majengo ya shule shilingi milioni 7," amesema Mghamba.

Amesema wamefanikiwa kuboresha mazingira ya shule kwa upandaji miti ya kivuli na matunda na kuongeza walimu wapya ili kuongeza nguvu kazi na kununua vitabu vya kiada, ziada na mitaala mipya ya ujifunzaji na ufundishaji.

Mwenyekiti wa jumuiya ya Nyanza Group, Kija Malimi, ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mahafali hayo kuwachangia fedha taslimu shilingi 600,000 amewapongeza wanafunzi hao kwa kufikia hatua hiyo.

Malimi amewaasa wazazi na walezi kuteketeza vyema wajibu wao katika kuhakikisha watoto wao wanapiga hatua kielimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...