Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Rungwe
MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hasan amewajibu wanaosema Chama hicho kinabeba wanachama wake kwenye magari kuwapeleka katıka mikutano ya kampeni zake ambapo amesema siyo shida wala siyo aibu kuwasafirisha wanaokwenda katika mikutano.
Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi wa Wilaya Rungwe mkoani Mbeya wakati wa mkutano wa kuomba kura kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu Mgombea Urais wa CCM Dk.Samia ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika mikutano ya Chama hicho.
“Nimeona Katibu wetu wa Itikadi na Uenezi wa Chama chetu ndugu Kenani akizungumza na Waandishi wa habari waliokuwa wakimwambia kwamba Chama Cha Mapinduzi mnasafirisha watu ndiyo mikutano yenu inajaa.
"Huwezi kutegemea mtu anatoka kilometa nyingi huko zaidi ya 80 ndani ya Rungwe atembee kwa miguu. Lazima tuwasaidie usafiri wafike lakini hatutoi watu wilaya nyingine kwenda wilaya nyingine.”
Dk.Samia wakati anaendelea kujibu hilo amesema kwamba kama wananchi wakiwemo wanachama wa CCM wana imani ya kwenda katika mikutano kusikiliza lazima wapewe imani ya kuwasogeza ili wafike kuwasikiliza.
“Kwahiyo siyo shida wala siyo aibu kwa chama kuwasafirisha wanachama wake kuja kusikiliza Ilani ya chama inasemaje lakini yale ambayo tumewatendea pia."
Ametumia nafasi hiyo mgombea huyo kueleza hatua kwa hatua mipango ya Serikali katika miaka mitano ijayo ambayo amesisitiza namna ambavyo wamejipanga kuendelea kuboresha huduma za kijamii katika maeneo yote na hasa vijijini kwa kutatua changamoto za wananchi.
Pia ameendelea kuwaomba wananchi kuichagua CCM katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu kwa kupiga kura ya Rais ,Wabunge na madiwani ili kuwa mafiga matatu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...