Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe , Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi leo Septemba 4,2025 amepokea taarifa ya maendeleo ya Chuo Kikuu Mzumbe na kufurahishwa na kasi ya maendeleo iliyofikiwa na Chuo kwa takribani mwaka mmoja tangu alipopokea taarifa ya mwisho mwezi Novemba 2024.
Akipokea taarifa hiyo jijini Dar es Salaam Dkt. Shein amempongeza mwenyekiti wa Baraza la chuo Kikuu Mzumbe Prof. Saida Yahya Othman kwa kuongoza vyema Baraza hilo ambalo ndicho chombo cha juu cha maamuzi na kusema kuwa Baraza limekuwa likisimamia vyema utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Chuo sambamba na kuipongeza Menejimenti nzima na Wafanyakazi ambao ameeleza kuwa wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kukiendeleza Chuo kwa weledi mkubwa chini ya uongozi mahiri wa Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. William Mwegoha
Pamoja na pongezi hizo Dkt. Shein amefurahishwa na jitihada za Chuo katika kushirikiana na taasisi mbalimbali. Kipekee amepongeza mpango wa Chuo wa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria kuandaa mtaala wa kufundisha Elimu ya Katiba, Uraia na Uzalendo katika Vyuo Vikuu nchi nzima, Chuo Kikuu Mzumbe kikiwa ndio waanzilishi. Amesisitiza mafunzo ya maadili na uzalendo kuwekewa mkazo kwa Wanafunzi na wafanyakazi ili Chuo kiendelee kupata maendeleo katika nyanja zote za kitaaluma na kijamii, lakini pia kuwawezesha vijana wa kizazi cha sasa kutambua wajibu wao katika kuheshimu na kulinda rasilimali na tunu za Taifa.
"Nimefurahishwa sana na taarifa yote hii, lakini natilia mkazo mafunzo ya maadili na uzalendo kwani ni masuala yanayoambatana, hivyo maadili yafundishwe pamoja na uzalendo nasi Chuo Kikuu Mzumbe tuchukue hatua za kuimarisha uzalendo wa nchi kwa vijana wa sasa". Alisisitiza Dkt. Shein.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Saida Yahya-Othman alimshukuru Mkuu wa chuo Kikuu Mzumbe kwa miongozo anayoitoa kila wakati anapopokea taarifa ya chuo na kusema kuwa hatua hiyo imekuwa ikitoa hamasa ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo jambo lililopelekea Chuo kuongeza kozi nyingi kwa muda mfupi na kujiongezea mapato ya ndani
Awali, akiwasilisha taarifa hiyo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha amesema kuwa Chuo kinaendelea na utekelezaji wa majukumu yake katika hali ya usalama na utulivu na amemshukuru Mkuu wa chuo kwa teuzi za viongozi wa juu aliowateua ambao ni Naibu Makamu Mkuu wa chuo - Taaluma, Utafiti na Ushauri pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Mipango, Fedha na Utawala na kutoa taarifa ya Baraza kuwateua viongozi kadhaa wa ngazi ya Menejimenti
Prof. Mwegoha ameeleza kuhusu mafanikio ya kuongezeka kwa ajira za Wafanyakazi na kuwaendeleza kitaaluma,kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi kwa asilimia 9.12, kuanzisha ushirikiano na Taasisi za ndani kwa kusaini mikataba ya ushirikiano 30 na mingine 45 ikiwa katika hatua za ukamilishwaji
Ameongeza kuwa chuo kimeendelea kuimarisha ushirikiano wa kimataifa ambapo hivi karibuni chuo kimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP wenye nia ya kukiwezesha chuo katika fursa za uwekezaji ikiwemo kutafuta fedha za ujenzi wa kituo cha uwekezaji eneo la Upanga katika Kampasi ya Dar es Salaam
Aidha, pamoja na mafanikio mengine ameeleza kuhusu kuendelezwa kwa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya kufundishia Kampasi kuu Morogoro na Tanga na hatua iliyofikiwa ya mradi wa hosteli za wanafunzi wa kike katika kampasi ya Mbeya
Viongozi mbalimbali pia walishiriki katika kikao hicho akiwemo Naibu Makamu Mkuu wa chuo Kikuu Mzumbe - Mipango, Fedha na Utawala, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Taaluma, Utafiti na Ushauri, Kaimu Katibu wa Baraza , Msaidizi Mahsusi wa Makamu Mkuu wa Chuo na Maafisa wa kitengo cha Mawasiliano na masoko wa Chuo kikuu Mzumbe

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha akikabidhi taarifa ya
maendeleo ya Chuo kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali
Mohamed Shein.
Mhe. Dkt. Shein akipokea taarifa hiyo tarehe 04 Septemba 2025 jijini Dar
es Salaam

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha akiwasilisha taarifa
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe ,Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akifuatilia taarifa ya Maendeleo ya Chuo iliyowasilishwa kwake na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Saida Yahya Othmani akifafanua jambo kuhusu uundaji wa kamati za mipango ya uwekezaji, shughuli za maendeleo .
Baadhi ya viongozi wa Menejimenti na Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe wakiwa katika kikao cha kukabidhi taarifa ya maendeleo ya chuo kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...