Na Mwandishi wetu,Longido
Shirika lisilo la kiserikali la Kilimanjaro Resource Centre (KRC) limegawa mizinga 100 kwa vikundi vya ufugaji nyuki katika kijiji cha Lerang’wa Tarafa ya Enduimet wilayani Longido, mkoa Arusha, ili kupunguza migogoro kati ya binadamu na Tembo na watumie mizinga hiyo, kama uzio ili Tembo wasiendelee kuvamia mashamba na kufanya uharibubu wa mali na vifo.
Kijiji hicho ni miongoni mwa vijiji vitano, vinavyopakana na hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, hifadhi ya Amboseli ya nchini Kenya na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Enduimet na vinatekeleza Mradi wa kuhifadhi na kurejesha ustawi wa maeneo ya mifumo ikolojia yaliyo hatarini kuathiriwa Kilimanjaro Magharibi na Longido (REPROTECT).
Akizungumza katika zoezi la kukabidhi Mizinga hiyo, lililotanguliwa na mafunzo ya wanavikundi na viongozi wa vijiji hivyo, Mkurugenzi wa shirika la KRC, Dkt. Gerubin Liberath Msaki alisema kupitia mradi huo wanatarajia kujenga uwezo wa jamii juu ya Shughuli za Ujasiriamali za uzalishaji Mali, ufugaji wa kisasa, kushirikiana jamii ili kukuza shughuli za utalii wa kitamaduni-ikolojia.

“Katika mradi huu pia tunatarajia kupanda miti, na kuendeleza jamii katika ufugaji wa nyuki wa kibiashara,kuwa na kilimo cha kisasa ili kuboresha maisha ya jamii katika Tarafa ya Enduimet”, alisema.
Dkt. Msaki alisema vijiji vingine vilivyopo katika mradi huo unaotarajia kunufaisha zaidi ya watu 15,000 ni, Kitendeni, Irkaswa, Kamwanga na Olmolog ambapo Katika mwaka wa Kwanza mradi utaanza katika Kijiji cha lerangwa kama sehemu ya jaribio la mradi (Pilot project) na baadae kuendelea katika vijiji vingine vya mradi katika mwaka wa pili na wa tatu.
Akikabidhi mizinga hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Longido, Jacob Lyimo aliwataka wananchi wa vijiji vitano, ambao wapo katika mradi huo, kutumia mradi huo kuboresha maisha yao lakini pia kukabiliana na migogoro baina yao na wanyamapori.
Lyimo ambaye ni mkuu wa kitengo cha Maliasili na Mazingira katika halmashauri ya Longido, alisema halmashauri kama mshirika wa mradi huo, itatoa ushirikiano kuhakikisha unaleta manufaa kwa jamii lakini pia kufatilia hatua zote za utekelezwaji wa mradi huo.
“Leo tunakabidhi mizinga hii mtumie vizuri katika ufugaji wa nyuki kisasa kwani licha ya kudhibiti tembo lakini pia mnapata asali ambayo mtauza na kupata fedha za kuboresha maisha yenu”,alisema.
Akitoa mafunzo ya kukabiliana na Wanyama wakali hasa Tembo, kwa wananchi wa vijiji hivyo Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori nchini (TAWIRI) Revocatus Meney alisema matumizi ya mizinga ya nyuki ndio njia bora zaidi kudhibiti uvamizi wa Tembo.
Alisema adui mkubwa wa Tembo ni nyuki, hivyo wananchi hao sasa watakuwa na uwezo wa kufuga nyuki na kupata asali lakini pia kudhibiti makundi ya tembo kuvamia mashamba yao na nyumba zao.
Hata hivyo, alieleza tabia mbali mbali za tembo kabla ya kufanya uvamizi na kusababisha uharibifu na vifo na kuwataka wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinaadamu ikiwepo kilimo na ujenzi katika maeneo ya mapito ya Wanyama hao.
“Hivi sasa kuna wilaya 91 Tanzania zinakabiliwa na migogoro ya Tembo lakini chanzo kikubwa ni wananchi kuongeza shughuli za kibinaadamu katika maeneo ya asili ya wanyamapori, lakini pia kulima mazao yanayovutia wanyamapori pembezoni mwa hifadhi, mapori ya akiba na hifadhi ya jamii za wanyamapori”, alisema.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Lerang’wa Isaya Lembura na mmoja wa wanakindi cha ufugaji, Obedi Mollel walishukuru wafadhili wa mradi huo, ambao unakwenda kuboresha maisha yao na kuahidi kusimamia mradi huo ili ulete mafanikio.
Lembura alisema serikali ya Kijiji chake, itatoa ushirikiano kwa mradi huo, kwani kwa miaka mingi wamekuwa na migogoro ya Tembo kuvamia mashamba yao na kufanya uharibifu mkubwa lakini sasa wanaamini Suluhu inapatikana.
Mradi huo wa miaka mitatu unatekelezwa na KRC pia unashirikisha taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Halmashauri za Wilaya Longido Mamlaka ya Misitu na Nyuki(TFS),Tanzania Forest Services (TFS) na Jamii za Wenyeji.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...