Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetoa elimu ya kimazingira na afya kwa vijiji viwili vya Mtonya na Mandela-Likuyu katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma kufuatia Mradi wa Uchimbaji wa Madini aina ya 'Uranium' unaotarajiwa kuanza hivi karibuni katika mgodi ulio karibu na vijiji hivyo.

Elimu hiyo imetolewa kwa wananchi kuanzia 8-9 Septemba, 2025 kwa vijiji hivyo huku ikifuatiwa na ukaguzi utakaofanyika katika mgodi huo ikiwa ni hatua ya awali ya kuelimisha jamii na wawekezaji kabla ya Mradi huo kuanza ambapo ni maagizo yaliyotolewa na Serikali ili kuhakikisha jamii inatambua uwepo wa Mradi huo na kuhakikisha jamii haiathiriki na Mradi huo.

Akizungumza katika utoaji wa elimu hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi, Kaimu Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria (NEMC) Bw. Jamal Baruti ameutaka Uongozi wa vijiji kutumia Kamati za Mazingira na kushirikiana na Serikali kuendelea kuelimisha jamii juu ya maswala ya Mazingira na Afya ya jamii yanayoweza kusababishwa na Mradi huo.

Kwa upande wake, Meneja Kanda ya Kusini (NEMC) Bw. Boniface Guni amewataka wakazi wa vijiji hivyo kuchangamkia fursa za ajira katika Mradi huo huku wakizingatia ulinzi wa Afya zao na Mazingira.

Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria NEMC Bw. Jamal Baruti amesema NEMC itaendelea na ufuatiliaji wa maswala ya kimazingira kwa kushirikiana na Taasisi nyingine huku akiitaka Kampuni ya Mantra TZ LTD ya Uchimbaji katika mgodi huo kutambua haki za wakazi wa vijiji hivyo na kuchangia shughuli za maendeleo ya wakazi wa vijiji hivyo kama manufaa ya Mradi huo.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...