Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Songwe

NI zamu ya Songwe kesho Septemba 3,hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea kwani mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya mikutano mikubwa ya kampeni mkoani Songwe.

Msafara wa Rais Dk. Samia unatarajiwa kuwasili leo kisha kuhutubia maelfu ya wananchi wa katika mikutano yake ya kampeni itakayofanyika Tunduma na Vwawa.

Maeneo mbalimbali ya miji hiyo imepambwa na bendera za CCM huku wananchi, wapenzi na wanachama wa chama hicho tawala wakiwa tayari kumsikiliza mgombea huyo wa Urais kupitia CCM.

Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Songwe, Komredi Yusuph Rajab, ameeleza kwamba mkoa huo umepanga kufanya mikutano itakayovunja rekodi kwa mapokezi.

"Tumejipanga vya kutosha kumpokea kiongozi wetu, mgombea Urais Dk. Samia kwani tutaweka historia kwa mapokezi makubwa.Wananchi wa Mkoa wa Songwe ni wanufaika wa miradi iliyotekelezwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. Samia.

Ametoa mwito kwa wananchi, wapenzi na wakereketwa wa CCM kujitokeza kwa wingi katika mikutano hiyo ya kampeni.Hata hivyo tangu mgombea Urais wa CCM ,Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuanza kampeni zake maelfu ya wananchi wamekuwa wakifika kumsikiliza akinadi Ilani na kutoa muelekeo wa Serikali atakayoiunda kuhusu yale anayokwenda kuyatekeleza.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...