MGOMBEA mwenza wa kiti cha urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi amepokelewa kwa shangwe na wananchi alipokuwa akiwasili katika uwanja wa CCM,wilaya ya Bariadi Vijijini mkoani Simiyu kuendelea na mkutano wa Kampeni, leo Jumatatu Septemba 1,2025.
Dk.Nchimbi aliyekuwa Mkoa wa Mara na sasa ameingia Mkoa wa Simiyu kuendelea na kampeni,akianzia jimbo la Busega na baadae kuelekea jimbo la Bariadi Vijijini na kufanya mikutano mikubwa ya hadhara.
Akiwahutubia wananchi wa Bariadi Vijijini mkoani Simiyu, Dkt.Nchimbi ambae ni Mgombea Mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, pia alimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi Vijijini,Masanja Kungu Kadogosa sambamba na wagombea ubunge wengine pamoja na Madiwani wa mkoa huo.
Dkt. Nchimbi anaendelea na kampeni zake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, ikiwa ni katika harakati za kuomba ridhaa ya Watanzania kuwaongoza katika awamu nyingine ya miaka mitano, katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa Kufanyika Oktoba 29, 2025.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...