Farida Mangube, Morogoro
Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi nchini (PSPTB) imeweka mikakati mipya ya kuboresha utendaji wake kwa mwaka wa fedha 2025/2026, baada ya kufanya tathmini ya bajeti na mafanikio ya mwaka uliopita, lengo likiwa kuongeza ufanisi katika sekta ya ununuzi na ugavi.
Akizungumza katika kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika mkoani Morogoro, Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB, Bw. Godfred Mbanyi, amesema kikao hicho kimekuwa fursa ya kupitia malengo ya mwaka uliopita na kupanga hatua za kufanikisha mipango ya mwaka ujao.
"Kikao hiki kinatupatia nafasi ya kuangalia tulipanga kufanya nini mwaka uliopita, kuona ni yapi tumetekeleza, ni yapi tumeshindwa na changamoto tulizokutana nazo. Hii itatusaidia kuweka mikakati mipya ya kuboresha utendaji kwa mwaka wa fedha 2025/2026," alisema Bw. Mbanyi.
Aidha, Bw. Mbanyi amebainisha kuwa mageuzi ya TEHAMA yamekuwa chachu ya kurahisisha mchakato wa usajili na mitihani ya kitaaluma, tofauti na awali ambapo kulikuwa na mlolongo mrefu wa urasimu ambapo hadi sasa, bodi imefanikiwa kusajili zaidi ya wataalam 10,000, huku mwaka 2024 jumla ya wanafunzi 680 walifanyiwa mitihani ya kitaaluma ikilinganishwa na lengo la wanafunzi 750.
"Bodi yetu inaendesha mitihani ya kitaaluma kwa wahitimu wa vyuo vikuu wa ununuzi na ugavi. Mitihani hii huwapa nafasi ya kupata vyeti vya kitaaluma vinavyowawezesha kufanya kazi kwa ufanisi na weledi katika taaluma hii," ameongeza Bw. Mbanyi.
Kwa upande wake, Katibu wa TUGHE tawi la PSPTB, Bi. Faraja Mgulambwa, amesema kikao hicho ni jukwaa muhimu kwa wafanyakazi kwani kinawawezesha kutoa maoni yao, kushirikiana na menejimenti, na kutafuta suluhu za changamoto zinazowakabili.
"Tumekutana hapa mkoani Morogoro kwa siku mbili katika kikao kazi kinachotupa mwanga wa kujadili mambo mbalimbali ya taasisi yetu na kutafuta suluhu za changamoto za kazi," alisema Bi. Mgulambwa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...