Katika kuendeleza dhamira yake ya kuchochea maendeleo ya kilimo nchini, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeendesha semina maalum kwa wakulima wa Mkoa wa Kagera, Wilaya ya Bukoba. 

Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa ELCT, ikiwa ni jukwaa la maarifa lililowakutanisha wakulima takribani 100 kwa lengo la kupata uelewa kuhusu huduma za kifedha zinazotolewa na Benki.

Kupitia mafunzo haya, wakulima walipata fursa ya kujifunza kwa kina kuhusu upatikanaji wa mikopo ya kilimo, huduma za uwezeshaji wa uzalishaji, na mbinu bora za kushiriki kikamilifu katika mnyororo wa thamani wa kilimo. 

Semina hii ni ushuhuda wa azma ya TADB ya kuendeleza kilimo chenye tija, jumuishi na endelevu kilimo kinachojenga maisha, jamii na uchumi wa Taifa.

Sambamba na semina hiyo, TADB inatarajia kufungua ofisi ndogo mkoani Kagera, hatua muhimu inayolenga kusogeza huduma karibu zaidi na wakulima, wafugaji, na wadau wa sekta ya kilimo. 

Uwepo wa ofisi hii utakuwa daraja la mawasiliano na ushirikiano wa karibu kati ya Benki na jamii ya wakulima, kwa lengo la kuharakisha upatikanaji wa huduma, kuongeza uwajibikaji, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kupitia kilimo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...