Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida, Ndg. Ahmed Misanga, ameendelea na harakati za kusaka kura za ushindi wa kishindo kwa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Singida Mjini.Misanga amekuwa akipita mtaa kwa mtaa na kijiwe kwa kijiwe akiwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi ifikapo Oktoba kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wagombea wa ubunge na udiwani kupitia CCM.Akizungumza na wananchi wa Singida Mjini, Misanga amesema:

“Ushindi wa CCM ni ushindi wa maendeleo. Ni jukumu letu kuhakikisha Mama Samia anaendelea kupewa nguvu ya kuongoza nchi, wabunge na madiwani wetu wapewe nafasi ya kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wananchi wa Singida.”

Amesisitiza kuwa mshikamano, mshikikano na kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi ni nguzo kuu ya kuimarisha chama na kulinda maslahi ya wananchi.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...