Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bara, Stephen Wasira ameungana na Mgombea mwenza  wa Urais Dkt. Emmanuel Nchimbi na viongozi mbalimbali kushiriki mazishi ya Mtoto wa Rais Mstaafu Hayati Ali Hassan Mwinyi, Abbas Ali Mwinyi yaliyofanyika Bweleo Zanzibar.

Mbali na kushiriki mazishi hayo, Wasira alitoa pole kwa Mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali ambaye ni ndugu wa marehemu Abbas Mwinyi.

Abbas Mwinyi alifariki dunia jana mjini unguja, na maziko yake yamefanyika leo Bweleo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...