Na Mwandishi wetu

Katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa chuo hicho, Profesa Ahmed Ame, amesema kuna umuhimu mkubwa wa kutumia takwimu katika kutengeneza sera za maendeleo ya taifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Septemba 1, 2025, wakati wa ufunguzi wa semina kwa waandishi wa habari, Prof. Ame amesema Serikali imepanua wigo wa matumizi ya takwimu katika upangaji wa maendeleo na kusisitiza kuwa takwimu sahihi ndizo msingi wa maamuzi bora.

“Takwimu ni namba ambazo haziongopi. Zinawawezesha wananchi kuelewa kwa usahihi kile kinachofanyika,” amesema Prof. Ame.

Alibainisha kuwa waandishi wa habari ni kundi muhimu katika usambazaji wa takwimu, kwa kuwa wao ndio wanaowafikia walaji wakuu wa taarifa, hivyo takwimu zinazotumika katika vyombo vya habari lazima zitokane na vyanzo vinavyotambulika kisheria.

Aidha, Prof. Ame amesema chuo hicho kimekuwa kitovu cha mafunzo na utafiti, kikihudumia nchi mbalimbali za Afrika, huku wakati mwingine wakufunzi wake wakitumwa kufundisha nje ya Tanzania.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika, Dkt. Tumaini Katunzi, amesema chuo kimekuwa kikizalisha wataalamu wa kutosha kwa ngazi ya shahada na shahada za uzamili, jambo linaloonesha matunda ya safari ya miaka 60 ya uwepo wa taasisi hiyo.

“Miaka 60 ya chuo hiki ni safari ndefu ambayo sasa imezaa matunda makubwa katika matumizi na tafsiri ya takwimu kwa maendeleo ya nchi na bara kwa ujumla,” amesema Dkt. Katunzi.
Mwenyekiti wa Bodi Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Prof. Ahmed Ame akizungumza katika Warsha ya waandishi wa habari iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo hicho Changanyikeni leo Septemba 1, 2025 Jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo imeandaliwa na Chuo hicho kwaajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu masuala ya Takwimu.
Mkuu wa Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Dkt. Tumaini Katunzi akizungumza katika Warsha ya waandishi wa habari iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo hicho Changanyikeni leo Septemba 1, 2025 Jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo imeandaliwa na Chuo hicho kwaajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu masuala ya Takwimu.

Mkuu wa Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Dkt. Tumaini Katunzi akizungumza katika Warsha ya waandishi wa habari iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo hicho Changanyikeni leo Septemba 1, 2025 Jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo imeandaliwa na Chuo hicho kwaajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu masuala ya Takwimu.

Makamu Mkuu wa Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Dkt. Indiael Kaaya akizungumza katika Warsha ya waandishi wa habari iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo hicho Changanyikeni leo Septemba 1, 2025 Jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo imeandaliwa na Chuo hicho kwaajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu masuala ya Takwimu.




Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika warsha iliyoandaliwa na Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kwaajili ya kujengewa uwezo kuhusu masuala ya Takwimu. Warsha hiyo imefanyika Changanyikeni leo Septemba 1, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Prof. Ahmed Ame akiwa na viongozi wengine wa chuo hicho wakipata picha ya pamoja na waandishi wa habari wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo waandishi hao kuhusu masuala ya takwimu. Warsha hiyo imefanyika Changanyikeni leo Septemba 1, 2025 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...