Morogoro – Watumishi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wamekutana kwa siku mbili mkoani Morogoro katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi kujadili utekelezaji wa shughuli za Mamlaka kwa mwaka wa fedha 2024/2025 pamoja na kuwasilisha na kuchambua mpango kazi wa mwaka 2025/2026.
Kikao hicho cha siku mbili kilichoanza Septemba 11 hadi 12, 2025 kimeongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Dkt. Erasmus Kipesha.
Katika kikao hicho, wajumbe walipata fursa ya kupokea taarifa za utekelezaji kutoka kwa vitengo mbalimbali vya Mamlaka, na kutoa maoni na mapendekezo ya namna ya kuboresha utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi zaidi.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho, Dkt. Kipesha alieleza kuwa Baraza la Wafanyakazi ni jukwaa muhimu linalowawezesha watumishi kushiriki moja kwa moja katika upangaji wa mipango na utekelezaji wa majukumu ya taasisi.
Alisisitiza kuwa ushiriki wa watumishi katika kujadili utekelezaji wa majukumu ya mamlaka na mikakati iliyowekwa kwenye utekelezaji ni msingi wa uwajibikaji, ufanisi na mafanikio ya taasisi kwa ujumla.
“Mkutano huu ni fursa mahsusi ya kujitathmini, kubadilishana mawazo, na kupanga kwa pamoja mikakati ya kuimarisha utendaji wetu ili kufanikisha malengo ya Mamlaka,” alisema Dkt. Kipesha.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA Dkt. Erasmus Kipesha akisisitiza jambokatika kikao cha tano kilichofanyika mjini Morogoro Septemba 11 na 12, 2025. Kulia niKatibu msaidizi Bw. Lusungu Kaduma.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA Bi. Mwanaisha Komba akitoa maelezo kwawajumbe wa baraza hilo katika kikao cha tano kilichofanyika mjini Morogoro kwa lengola kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji na kiutumishi.

Kaimu Mkurugenzi Utafutataji Rasilimali na Usimamizi Miradi ya Elimu Bw. Masozi Nyirenda akitoa ufanunuzi kuhusu utekelezaji wa miradi ya elimu kwa wajumbe waBaraza la Wafanyakazi wa TEA mjini Morogoro.
Meneja Huduma za Sheria kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Christina Meela (katikati)akitoa taarifa ya utekelezaji kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi waTEA katika kikao kilichofanyika mjini Morogoro.

Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi CPA. Mwanahamis Chambega akitoa maelezo kuhusuutekelezaji wa bajeti ya mamlaka kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA katika kikao cha tano kilichofanyika mjini Morogoro.
Kaimu Meneja Usimamizi wa Miradi ya Elimu Bi. Mwafatma Mohamed akijibu maswaliya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA walipokutana mjini Morogoro kupitia nakujadili taarifa za utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo.

Mkaguzi Mkuu wa Ndani CPA. Richard Mazinge akitoa maelezo kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA kwenye kikao cha tano kilichofanyika mjini Morogoro kwalengo la kupitia na kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji za mamlaka. Kushoto niMkurugenzi wa Huduma za Taasisi CPA. Mwanahamis Chambega.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA Dkt. Erasmus Kipesha (kulia) pamoja naKatibu wa Baraza hilo Bi. Mwanaisha Komba (kushoto) wakifuatilia taarifa na maonikutoka kwa wajumbe wa baraza hilo wakati wa kikao cha tano kilichofanyika Morogoro.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Pili la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wakifuatiliauwasilishwaji wa taarifa za utekelezaji katika kikao cha tano cha baraza hilokilichofanyika mjini Morogoro.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Pili la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wakifuatiliauwasilishwaji wa taarifa za utekelezaji katika kikao cha tano cha baraza hilokilichofanyika mjini Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...