Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele leo Septemba 21, 2025 ametembelea Halmashauri ya Mji wa Mafinga Wilayani Mufindi Mkoani Iringa ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ambapo pamoja na mambo mengine alipokea taarifa ya Mji huo kutoka kwa wasimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025 na kisha kukagua vifaa ambavyo tayari vimepokelewa katika Halmashauri hiyo.


Jaji Mwambegele yupo Mkoani Iringa kukagua maandalizi hayo na kutazama kampeni za wagombea katika majimbo ya Mkoa wa Iringa



kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na Tume,Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.

"Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura"
Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Iringa Bi. Nuru Sovella akizungumza jambo wakati wa utoaji wa taarifa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele
Msimamizi Jimbo la Mafinga Mjini Mwalimu Doroth Kobelo akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele (katikati) kulia ni Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Iringa, Bi. Nuru Sovella.


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na wasimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mafinga Mjini ambapo aliwasisitiza kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi.


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na wasimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mafinga Mjini ambapo aliwasisitiza kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi.

Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Iringa, Bi. Nuru Sovella akisikiliza kwa umakini


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akiangalia sehemu ya vifaa vya uchagzi ambavyo vimeshapokelewa.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...