Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Songwe

WAGOMBEA ubunge wa majimbo yaliyopitishwa katika Mkoa wa Songwe wametaja mafanikio lukuki yaliyofanywa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka minne na nusu ya uongozi wake huku wakitumia nafasi hiyo kuahidi kwa niaba ya wananchi wakiahidi kumpigia kura Rais Samia katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.

Akizungumza leo Septemba 3,2025 katika mkutano wa kampeni za mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ,mgombea ubunge wa Jimbo la Tunduma,David Silinde amesema wanamshukuru Rais Samia  kwa sababu katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake amefanya mambo makubwa.

Amesema katika sekta ya  elimu amewapatia fedha  Sh bilioni 28  kwa ajili ya elimu msingi na sekondari pamoja na ujenzi wa shule mpya saba za ghorofa ikiwemo shule ya mfano ya Dkt Samia iliyogharimu Sh.bilioni 6.

Kwa upande wa afya Silinde amesema walikuwa na kituo kimoja cha afya cha Tunduma lakini chini ya Rais Samia sasa vipo vitano na vyote vinafanya kazi pamoja na sh bilioni 9.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji.

Silinde amesema kuwa katika barabara za ndani  ya Jimbo hilo kulikuwa na mtandao wa kilometa  1.7 lakini kwa sasa zipo  kilometa 10.7 ambazo zimejengwa kwa Sh.bilioni 5.6.

Kuhusu mikopo ya vijana,wanawake na wazee, amesema kuwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amewapatia fedha Sh.bilioni 8.113.

Akizungumza kuhusu vyanzo vya mapato ameeleza wakati anaingia madarakani walikuwa wanaingiza  Sh.bilioni  4.8 na sasa wanakusanya fedha Sh.bilioni 22.8.

Pia amesema amani kwa mji wa Tunduma kwa sasa ni kubwa sana na sababu ya kuwepo kwa amani na utulivu msingi wake ni Rais Samia Suluhu Hassan.”Sababu ya Tunduma kuwa na amani kwa sasa ni kutokana na Rais Samia kupeleka  fedha za Maendeleo katika Jimbo la Tunduma.”

Akizungumzia sekta ya maji Silinde amesema  wanatekeleza miradi nane yenye thamani ya fedha Sh bilioni 5.1 ambapo mahitaji yalikuwa   lita milioni 8 lakini kupitia mradi huo watapata lita milioni 20.

Kwa upande wake Mgombea Ubunge Viti Maalum Jimbo la Songwe,Juliana Shonza amesema kuwa wananchi wa Mkoa huo wanayo furaha kubwa kutokana na mkoa huo kuunganishwa katika umeme wa grid ya Taifa hivyo kwa sasa wana umeme wa uhakika.

“Vitongoji 800 vimeunganishwa na umeme vimebaki 500 ambapo tayari katika bajeti vitafikiwa  vijiji 250.Wanawake Mkoa wa Songwe wamejipanga kuhakikisha Rais Samia anapata kura za kishindo na wapo imara kuhakikisha njia yake inakuwa nyeupe katika ushindi.”

Wakati huo huo Mgombea wa Jimbo la Mbozi,Onesmo Mkondya pamoja na kumhakikishia Rais Samia kuwa wananchi wanakwenda kumpa kura kwa kwenda kutiki Oktoba 29,2025 ametumia nafasi hiyo kumuomba Rais Samia kuendelea kutoa ruzuku ya mbolea na pembejeo kwani tegemeo lao lipo katika kilimo.

Kwa upande wake Mgombea  Ubunge Jimbo la Momba,Condester  Sichalwe amemuomba  Rais Samia awapatie kituo cha forodha ili mapato ya ndani katika halmashauri yaongezeke ili kusaidia katika kutekeleza miradi midogo midogo.

"Nikiwa Bunge I baada ya kumalizika Uchaguzi Mkuuu nataka nikiwa bungeni niwe naomba miradi mikubwa.Katika miaka minne nyuma tulikuwa tunakusanya fedha Sh.bilioni 1.1 na sasa tunakusanya Sh.bilioni 3.5.

“Tunaamini tukipata geti hata ile mikopo ya asilimia 10 tutaweza kulipa,"alisema Condester na kufafanua maendeleo ambayo Rais Samia amepeleka katika Jimbo hilo kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wake ni sawa na miaka 10.

“Yamejengwa madarasa  107 katika shule za msingi na  109 sekondari  kwenye shule 11 kwenye Kata 14 ambapo Kata  zote 14 zina shule na mbili  za ziada.Sekta ya maji kabla ya miaka minne ya Rais Samia tulipokea fedha Sh.bilioni 3 na kwa sasa tunapatiwa  Sh bilioni 21.6












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...