NA MWANDISHI WETU

Young and Alive Initiative kwa kushirikiana na Community Consortium Uganda wamezindua rasmi mradi wa miaka mitatu wa Obstacle Race Against Stigma and Shame (ORASS) wenye lengo la kupunguza unyanyapaa na kukuza ustawi wa vijana nchini.

Mradi huo unawalenga vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 katika shule mbili za msingi na sekondari tatu zilizopo mikoa ya Tabora, Mbeya na Dar es Salaam.

KUJENGA UELEWA WA JAMII

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi wa Young and Alive Initiative, Secilia Shirima, alisema mradi huo utaanza kutekelezwa kwa miezi 15 ya awali kwa lengo la kujenga uelewa miongoni mwa wanafunzi, wazazi na jamii kuhusu changamoto za afya ya akili.

“Wanafunzi wengi huonekana wako salama, lakini changamoto za kiakili haziwezi kutambuliwa bila msaada wa kitaalamu. Wazazi na walimu watajengewa uwezo wa kutambua dalili, kusaidia matibabu na kutoa ushauri nasaha,” alisema Shirima.

UBUNIFU WA MRADI

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mradi kutoka Community Consortium Uganda, Alice Male, alisema ORASS ni ubunifu unaochanganya michezo, mafunzo ya vitendo na elimu ya afya ya akili kwa lengo la kupunguza kwa asilimia 70 unyanyapaa unaohusiana na matatizo ya kiakili miongoni mwa vijana.

SERIKALI YAPONGEZA

Akizungumza kwa niaba ya serikali, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais–TAMISEMI anayeshughulikia Elimu kwa Wenye Mahitaji Maalum, Ernest Hinju, alisema serikali inaunga mkono mradi huo kwa kuwa utasaidia kupunguza unyanyapaa na kuongeza uelewa kuhusu matatizo ya afya ya akili.

“Serikali inaamini kupitia mradi huu jamii itakuwa na mwamko wa kutambua changamoto za kiakili, kupata matibabu stahiki na kuachana na imani potofu zinazochangia kunyanyapaa wagonjwa,” alisema Hinju.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...