Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Arusha

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ameeleza  katika miaka mitano ijayo Serikali imejipanga kuboresha miundombinu mbalimbali ya mji wa Arusha ikiwemo masoko ya kisasa na barabara za lami.

Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Arusha leo Oktoba 2,2025 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ,Dk.Samia amesema kwa muda mrefu jiji hilo la Arusha lilikuwa halina stendi ya sasa lakini sasa tayari ujenzi umeanza takribani sh. bilioni 14.3 zinatumika katika mradi huo uliopo Bondeni City.

Pia, amesema  katika eneo hilo la Bonden City Serikali inakwenda kujenga soko kubwa la wafanyabiashara wadogo maarufu kama Machinga.

“Katika kipindi cha miaka mitano tumejenga soko la Mbauda kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo. Vilevile tutaendelea na ujenzi wa masoko mawili mengine eneo la Morombo na Kilombero kwa thamani ya Sh.bilioni 30.6.”

Pia amesema Kwa Arusha amesema tayari vikundi 853 vya wajasiriamali vimenufauka na zaidi ya Sh.bilioni 10.4 zimetumika huku serikali ikijipanga kuanzisha mfuko maalum kwa wafanyabiashara ndogondogo.

Kuhusu mahitaji ya maboresho ya barabara za ndani ya Jiji  la Arusha ambapo jiji hilo limejumuishwa katika mradi wa TACTIC ambapo jumla ya kilometa 10.2 zitajengwa kwa kiwango cha lami.

Baadhi ya barabara hizo ni Oljoro kilometa 4.7, Engosheraton kilometa 4.8, Olasiti kilometa 4 ambazo zitajengwa ili Jiji la Arusha lipate hadhi yake ya kuwa jiji hasa ukizngatia watalii zaidi wanafika katika jiji hilo.“Reli za kisasa zitakuja hivyo lazima jiji hilo liwe na mtandao wa barabara za lami.”








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...