ALAF Limited, kampuni inayoongoza katika suluhisho mbalimbali za ujenzi nchini, leo imezindua rasmi msimu wa nane wa ligi yake ya mpira wa miguu ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kampuni hiyo wa kukuza afya bora miongoni mwa wafanyakazi.
Ligi hiyo, ambayo imeshajizolea umaarufu mkubwa hadi sasa, itahusisha wafanyakazi wa ALAF kama wachezaji watakaounda timu tano yaani Simba Dumu, Simba Chuma, Maxcover, Safcool na Safthem yote yakiwa ni majina ya bidhaa zinazozalishwa na ALAF.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Afisa Mtendaji Mkuu wa ALAF, Bibhu Nanda alisema mbali na kukuza utamaduni wa michezo ligi hiyo pia ni sehemu ya kampuni hiyo kuhakikisha wafanyakazi wanazingatia afya bora na mazoezi ili waendelee kuzalisha zaidi na kuishi maisha bora.
“ALAF tunajali sana afya za wafanyakazi wetu ndio maana tukaamua kuanzisha ligi hii ya mpira ikiwa ni miongoni mwa michezo mingine mbalimbali amabyo wafanyakazi wetu hushiriki,” alisema.
Alisema mazoezi na michezo kwa ujumla inasaidia pia kupunguza magonjwa mbalimbali miongoni mwa wafanyakazi. “Hii sambamba na kuboresha na kulinda afya zetu wote, pia ni njia nzuri ya kudumisha ushirikiano na mshikamano miongozi mwa wafanyakazi.,” alisema.
Juma Ndabile, Afisa Mtendaji Mkuu wa Don Chief Sports Promotion, ambaye kampuni yake ndio mratibu wa ligi hiyo kwa niaba ya ALAF, alisema mipango yote imekamilika tayari kwa kuanza kwa ligi hiyo Jumamosi Oktoba 11, 2025 katika Viwanja vya Polisi Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Alithibitisha kuwa jumla ya mechi 24 zitachezwa katika mzunguko wa kwanza na wa pili na kwamba timu nne bora zitasogea katika hatua ya nusu fainali na baadaye timu mbili zitacheza mechi ya fainali Desemba 9, 2025 katika viwanja vya polisi Kurasini.
Kwa upande wake, Kululinda Emmanuel, ambaye ni Mwenyekiti wa Mpira wa Miguu ALAF alisema, “Ligi hii ilikuwa na ushindani mkubwa msimu uliopita jambo ambalo linatufanya tutegemee msimu mzuri mwaka huu wenye msisimko mkubwa, Lengo letu ni kutengeneza timu moja inayoiwakilisha ALAF katika michezo mbalimbali huku pia tukidumisha umoja miongoni mwa wafanyakazi.”
Aliendelea kusema kuwa uwekezaji katika afya bora ya wafanyakazi ni mkakati wa muda mrefu wenye lengo la kukuza uzalishaji na ustawi wa wafanyakazi.
Bingwa watetezi wa ligi hii ni Simba Dumu ambao walichukua kombe hilo kutoka kwa Safcool. Safbuild ambao walitetea kombe hilo kwa misimu mitatu mfulululizo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa ALAF Limited, Bibhu Nanda (kulia), akiwakabidhi mpira manahodha wa timu zitakazoshiriki Ligi ya ALAF inayoanza Jumamosi hii, Oktoba 11,2025 Jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Alaf Limited, Bibhu Nanda (kulia), akimkabidhi Jezi Nahodha wa timu ya Saf Cool, Addo Mahay, wakati wa uzinduzi wa Ligi ya ALAF Jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2025
Baadhi ya viongozi wa Kiwanda cha kuzalisha mabati cha ALAF wakiwa katika Uzinduzi Ligi ya ALAF uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 11,2025
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...